SI KWELI Mbowe: Tumeshindwa, tuelekeze nguvu zetu uchaguzi Ujao

SI KWELI Mbowe: Tumeshindwa, tuelekeze nguvu zetu uchaguzi Ujao

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Tumeshindwa,tuelekeze nguvu zetu uchaguzi Ujao

1733898851203.png
1733898877007.png

1733898886412.png
1733898899220.png

1733898908393.png

 
Tunachokijua
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama cha kisiasa nchini Tanzania ambacho kuanzia mwaka 2010 kilikuwa chama kikuu cha upinzani.

Kilianzishwa tarehe 28 Mei 1992 na mwanasiasa mkongwe Edwin Mtei, aliyewahi kuwa waziri wa fedha katika miaka 1977 hadi 1979.

Mbowe: Tumeshindwa, tuelekeze nguvu zetu uchaguzi Ujao

Desemba 10, 2024 CHADEMA kupitia Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, waliitisha Mkutano na Waandishi wa Habari kutoa Maazimio ya Kikao cha Kamati Kuu walichoitisha kwa Dharura Novemba 29, 2024 ili kujadili mchakato wa Mwendendo wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mpaka kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo na nini wanakusudia kufanya kama maazimio yao kama Chama.

Kufuatia Mkutano huo, Kumeibuka Posta zinazodaiwa kuwa ni za Jambo Tv na The Chanzo zinazodaiwa kuchapisha Taarifa kuwa kwenye mkutano wa CHADEMA na Waandishi wa Habari kuwa Mbowe alisema: Tunakwenda kujipanga tena kwa sasa tumeshindwao kupitia Jambo Tv , na nyingine ya The Chanzo ikidai kuwa Mbowe amesema Vijiji vingi havikusimamisha wagombea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, na hicho ndicho kimeathiri wao kupelekea kushindwa.

Aidha, nyingi ya Jambo Tv inasema, "Badala ya kutafuta wa kulaumiwa, ni bora kuelekeza nguvu zetu kwenye kwenye maandalizi ya achaguzi Mkuu wa 2025. Tumeshindwa safari hii, lakini ni nafasi ya kujipanga upya na kurejea tukiwa imara zaidi", - Mbowe (Tazama hapa, hapa)

Je, uhalisia wa Madai hayo ni upi?
JamiiCheck Imefatilia Mkutano wa CHADEMA na Waandishi wa Habari uliofanyika, leo Desemba 10, 2024 Makao Makuu ya CHADEMA na kubaini kuwa Kauli zinazodaiwa kutolewa na Mbowe kuwa wamekubali kushindwa na wanajipanga na Uchaguzi ujao Si za kweli.

Aidha, kwenye mkutano huo, CHADEMA wamesema uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 ulikuwa umegubikwa na uvunjifu wa kanuni na sheria za uchaguzi huku nguvu za Dola zikitumika kusaidia Wizi wa kura na hivyo kufanya kukosekana kwa haki kwa vyama vya Upinzani kwenye uchaguzi huo, Kutokana na hilo wamesema Hakuna Uchaguzi tena kama hakuna mabadiliko(No Reform No Election)
GecravvXsAAK01P
Ni upi uhalisia kwamba Mbowe amesema atagombea tena nafasi ya uenyekiti CHADEMA pamoja na Urais 2025?

Katika mkutano huo na waandishi wa habari Mbowe hakusema moja kwa moja kwamba atagombea nafasi ya uenyekiti ndani ya chama hicho wala Urais 2025 isipokuwa alisema muda utasema na atakayeamua kama Mbowe atagombea au hatagombea ni chama chake

“Mimi sijasema nagombea, si msubiri tu muda useme, shida iko wapi sasa, ingekuwa kutokusema kwangu ningekuwa nimemzuia mtu yeyote asiseme, hilo lingekuwa jambo jingine, vitu vingine vinapikwa ndani jamani viacheni vipikwe viive”

"Unasema mbowe ondoka, watakaoniambia Mbowe ondoka ni wana-CHADEMA, hawa watakaoniambia Mbowe gombea ni wanachama hawa, na viongozi wangu hawa yutaelewana mambo yetu ya ndani yanawahusu nini?, mimi nashangaa tu huko mitandaoni pilipili usiyoila inakuwashia nini?"
Mbowe alisema Tazama hapa kuanzia 1:19:45 hadi 1:21:13

Aidha chapisho hilo halijachapishwa na kurasa rasmi za mitandao ya kijamii, za Jambo TV bali alama na utamulisho wake vimetumika kutengeneza taarifa hiyo inayopotosha.

Je, ni upi uhalisia juu ya kauli inayodaiwa kutolewa na Makamu mwenyekiti wa chama hicho Tundu lissu kwamba alisema Safari iliyopo mbele ni ngumu kweli kweli, inahitaji viongozi wasafi, inahitaji viongozi wenye msimamo, inahitaji viongozi wasionunulika, inahitaji viongozi jasiri?

Ufuatiliaji wa JamiiCheck ulibaini kuwa kauli hiyo haikutolewa na Lissu katika mkutano huo katika muda wote alipopata nafasi ya kujibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali. Hata hivyo chapisho lilikuwa na taarifa hiyo halikuchapishwa katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya Swahili Times.
Madai ya Mbowe kusema ni vigumu kumuelewa mtu anayesema maridhiano hayajazaa matunda kutokana na kurejesha baadhi ya nafasi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa

Kumekuwepo na grafiki yenye nembo ya jambo ya Jambo Tv ikisomeka

“MWAKA 2019 TULIPOTEZA VIJIJI, NA MITAA LAKINI MWAKA HUU TUMEFANIKISHA KUREJESHA NAFASI HIZO. KWA HALI HII NI VIGUMU KUELEWA MTU ANAYESEMA MARIDHIANO HAYAJAZAA MATUNDA”. Taarifa hiyo imehifadhiwa hapa.

JamiiCheck imefuatilia madai hayo na kubaini si ya kweli na hayajotelewa na Jambo Tv kwani hayapo katika kurasa rasmi za Jambo Tv. Aidha tumefuatilia mkutano wa Mbowe na waandishi wa habari wa tarehe 10-12-2024 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Mbowe aligusia suala la uchaguzi wa mwaka 2019 ambapo alisema;

“Mwaka 2019 tulisimamaisha wagombea vilevile nchi nzima siwezi kusema ni asilimia 100, lakini tulisimamisha wagombea wakaenguliwa mapema kabisa tukaamua kujitoa kwenye uchaguzi na vyama vingine vya upinzani vikajitoa kwenye uchaguzi. CCM hawakujali wakasema asante Mungu wakapita bila kupingwa. Kwahiyo kwa kiwango kikubwa hatukapata muda wa kujifunza na kuona kwa macho yetu wenyewe uhalisia wa uchaguz. Mwaka huu tuliposema tutashiriki bila kujali makosa yatakayofanyika ili tuone kwamba linyeshe tuweze kujua panapovuja, na kweli tumeona panapovuja”

Mbowe hakugusia suala la maridhiano alipozungumzia suala la uchaguzi wa mwaka 2019 na badala yake alieleza kuwa walijitoa mwaka 2019 lakini kwa mwaka huu 2024 waliona ni bora washiriki ili kuona hali itakavyokuwa.

Je ni upi uhalisia wa Taarifa juu ya uwepo wa mkutano mwingine wa Lissu na Waandishi wa habari?
Aidha kabla ya mkutano huo na waandishi wa habari uliorushwa mbashara na vyombo mbalimbali vya habari nchini kuliibuka upotoshaji kupitia chapisho lililotengenezwa likieleza uwepo wa mkutano mwingine wa Lissu na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena muda sawa na mkutano wa Mbowe, hata hivyo JamiiCheck ilibaini kuwa taarifa za chapisho hilo si za kweli kwani hazikutolewa na CHADEMA na Lissu alikuwepo kwenye mkutano wa Mwenyekiti Mbowe.
Back
Top Bottom