Elections 2010 Mbowe: Tutashirikiana na Kambi ya Upinzani Bungeni

Elections 2010 Mbowe: Tutashirikiana na Kambi ya Upinzani Bungeni

While it's a good idea for opposition in the union parliament to join hands and fight for the common cause, the political atmosphere in Zanzibar at present leaves one with a lot of questions on reliability of CUF as credible opposition.

Sote tunajua kuwa CUF ina nguvu zaidi Zanzibar na hivyo ingawa Lipumba ni m/kiti, ushawishi wa viongozi kutoka ZNZ ndani ya CUF ni mkubwa zaidi hasa ukizingatia kuwa wao sasa ni sehemu ya dola wakiwa na nguvu zaidi ya kisiasa na hata kiuchumi

Itakuwaje inapotakiwa kutoa msimamo wa upinzani ktk jambo ambalo serikali ya muungano CCM na serikali mseto CCM na CUF zina maslahi?

Niliwahi kusoma kwenye MWANAHALISI, ilielezwa kuwa CHADEMA waliomba CUF itoe mgombea mwenza na CHADEMA itoe mgombea urais ili washirikiane, lakini wakati hilo linajadiliwa, Kikwete aliwapigia simu viongozi CUF zanzbr na kuwaambia kama wanataka kweli kuunda serikali ya pamoja visiwani na CCM, waondoe wazo la kuungana na CHADEMA bara vinginevyo watakosa kote. Akina Maalim Seif kwa kulinda "kitumbua chao" wakafuta wazo la kuungana na CHADEMA. Je, hili la mgongano wa maslahi haliwezi kujirudia ndani ya bunge?

Isitoshe,wapinzani wengine kama Mrema, Cheyo, Mbatia "wameshachakachuliwa". Hawa badala ya kuunga mkono wapinzani wenzao, wamekuwa wakiwasakama na huku wakiisifia CCM na Kikwete. Je? Hawa ni wa kuungana nao? Au mnataka bora wingi,muonekane mnafika 100 huku mamluki kibao kati yenu?


Mimi naona hapa kuna point lazima chadema tuwe makini, hamna haja ya kuwa wengi huku mamluki kibao. Hamad Rashid binafisi ninampenda na anafaa kuwa kiongozi lakini kwa uswahiba wa CCM na CUF kwa sasa sijui kama haitakuja kula kwao Chadema kama wataungana na CUF.
Ni kweli kwa kutegemea uzembe wa CCM wa kumteua Mgombea wao wa SPIKA, Upinzani unaweza kuchukua kiti hicho lakini ni kwa bahati tu.
Mimi kwa mtazamo wangu pia ndoa ya CHADEMA na CUF inaweza kuwa sumu iliyotegwa na CCM kutumaliza. Nashauri Chadema tuwe waangalifu sana na jambo hili kwa sasa. Nadhani Kamanda mbowe ameshasema kwamba ni kile chama makini chenye nia ya dhati ya kuwatumikia watanzania ndicho tushirikiane nacho!
 
hembu nifahamisheni, dr. Slaa anakwenda dodoma kama nani? Kwani yeye ni mbunge? Na inamaana sasa slaa amekubali matokeo na kuitambua serikali ya ccm? Kama hajaitambua bado inakuaje chadema waende dodoma? Unapohudhuria vikao vya bunge ni lazima ujadili bajeti ya serikali na kama huitambui serikali yenyewe hapo ni kichekesho!!!

chadema ni lazima wawe na msimamo ili wananchi tusiyumbe! Kama slaa hajakubali matokeo mbona anaelekea dodoma kwenye bunge?

naomba ufafanuzi hapa!!
kweli ujinga ni mzingo, kuliko hata gunia la lumbesa! Kwani hata wewe unakatazwa kwenda dodoma? Kwani dodoma sio sehemu ya tanzania!!? Watu makini huwa hawafanyi maamuzi kwa kukurupuka, cuf ndio walikuwa wanakurupuka na kususia bunge matokeo yake yaliwaghalimu, sasa usidhani dr slaa ni kilaza, akurupuke tu, pole ndugu, jiulize swali moja la msingi kwa nini mpaka leo barrack obama ajatuma salamu za pongezi kwa kikwete? Think.
 
What i m trying to count on ni kuwa, iwapo ccm watalazimisha kumpitisha chenge kama mgombea wao, kuna uwezekano mkubwa wa wabunge wengi wa ccm kumpigia mgombea tofauti na wa kwao. (wana ccm wengi tu wamewapigia opposition candidates ktk uchaguzi ulioisha). Hivyo basi, CHADEMA wakimweka Marando, au wamsupport Rashid, anything may happen.
Angalizo tu, Rashid as an individual sina tatizo naye, hajawahi kuweka upinzani wake in doubt. kitendawili ni kitu gani kitakuja baada ya CUF kuuungana ccm hivi karibuni, can they be trused? wanaweza wakauza timu hawa. It's better for CHADEMA to go it alone, (kwenye uspika) kuliko kuwategemea CUF.

kaka si vyema chadema waende kivyao washiikiane na CUF kwenye isshu ya Uspika, mtu kama Hamad Rashid ana heshima zake na pia ni mtu mwenye hofu ya Mungu siamini kama anaweza kununulika kirahisi.
 
Back
Top Bottom