Elections 2010 Mbowe: Tutashirikiana na Kambi ya Upinzani Bungeni



Mimi naona hapa kuna point lazima chadema tuwe makini, hamna haja ya kuwa wengi huku mamluki kibao. Hamad Rashid binafisi ninampenda na anafaa kuwa kiongozi lakini kwa uswahiba wa CCM na CUF kwa sasa sijui kama haitakuja kula kwao Chadema kama wataungana na CUF.
Ni kweli kwa kutegemea uzembe wa CCM wa kumteua Mgombea wao wa SPIKA, Upinzani unaweza kuchukua kiti hicho lakini ni kwa bahati tu.
Mimi kwa mtazamo wangu pia ndoa ya CHADEMA na CUF inaweza kuwa sumu iliyotegwa na CCM kutumaliza. Nashauri Chadema tuwe waangalifu sana na jambo hili kwa sasa. Nadhani Kamanda mbowe ameshasema kwamba ni kile chama makini chenye nia ya dhati ya kuwatumikia watanzania ndicho tushirikiane nacho!
 
kweli ujinga ni mzingo, kuliko hata gunia la lumbesa! Kwani hata wewe unakatazwa kwenda dodoma? Kwani dodoma sio sehemu ya tanzania!!? Watu makini huwa hawafanyi maamuzi kwa kukurupuka, cuf ndio walikuwa wanakurupuka na kususia bunge matokeo yake yaliwaghalimu, sasa usidhani dr slaa ni kilaza, akurupuke tu, pole ndugu, jiulize swali moja la msingi kwa nini mpaka leo barrack obama ajatuma salamu za pongezi kwa kikwete? Think.
 

kaka si vyema chadema waende kivyao washiikiane na CUF kwenye isshu ya Uspika, mtu kama Hamad Rashid ana heshima zake na pia ni mtu mwenye hofu ya Mungu siamini kama anaweza kununulika kirahisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…