Hellow Tanganyika!!
Uliyoyasikia kuhusu wewe kuchoka Si mwili pekee, Bali Fikra za kuleta uono Mwema wa chama na Nchi chini ya uongozi wako.
1. Kupoteza kumbukumbu ni kiashiria kikuu Cha Mkt Mbowe kuchoka, Ndugu Mbowe umeshasahau kuwa Mwaka 2014 chama chako kimekuwa mstari wa mbele kudai katika mpya na kuheshimu maoni ya wananchi kwamba kuwepo na ukomo wa uongozi katika ngazi zote, watu wastaafu umri ukifika waingie Damu changa na Fikra mpya. Sasa iweje tudai Katiba mpya ilhali iliyopo imeweka ukomo wa Rais kukaa mamlakani wakati CHADEMA hakuna ukomo Kwa nafasi ya mkt wa chama Kwa muda wa uongozi?
2. Ujio wa Lowwassa CHADEMA ulichangia Kwa kiasi kikubwa kuchafua image ya chama mbele ya umma. Haya yote yametokea Ukiwa mkt wa chama.
3. Kuingia na kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024, ni Moja ya mapungufu ya uongozi wako, kushindwa Kwa chama chako ni mapungufu ya uongozi wako, yalitokea mambo hayo hayo chini ya Magu 2019, na kwann hukujifunza ukarudia Yale Yale Yale 2024?
4. Kushindwa Kwa maridhiano uliyokiaminisha chama ni mapungufu Yako binafsi kama kiongozi, uliwaamini vipi CCM na kumsafisafisha mkt yule wa upande wa pili Hadi kumwalika Moshi kwenye sherehe za Bawacha?
5. Kuingia katika maridhiano bila idhini ya chama ni jambo la kutiliwa shaka pia, kwanini hukuomba ruhusa uende kwanza nyumbani, ubadili nguo, Kisha uonane na wanachama na viongozi Kisha yafanyike maamuzi ya kuingia katika meza ya maridhiano na CCM? Kwanini kupiga GIA ya angani Toka gerezani Hadi jumba jeupe?
6. Jitihada zako kukemea RUSHWA ndani ya chama ni za chini sana, matumizi na vipaumbele katika matumizi ya pesa za chama pia ni dhaifu, hayo pia ni mapungufu yanayokuhusu kama Mwenyekiti wa CHADEMA.
Ndugu Mbowe, baba Yako wa Ubatizo Mwl Nyerere aliachia Urais kukiwa hakuna mtu maarufu kumzidi, na alikuwa na nguvu pia na uwezo kifikra kuendelea kuwa Rais wa Nchi.
Ushauri: Jitoe mbele ya safari kipindi Cha compaign au subiri MAPINDUZI Toka Kwa vijana Rika la kina Sativa.
Mungu ibariki CHADEMA.
Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
Karibuni 🙏