Pre GE2025 Mbowe umechoka katika fikra zaidi kuliko mwili

Pre GE2025 Mbowe umechoka katika fikra zaidi kuliko mwili

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huwi mwanachama wa chama fulani sabab unataka kuwa kiongozi..na kwa Tanzania ni vigum sana kupata watu aina ya Mbowe..uvumilivu, kujitoa, kuwa mlezi, na msimamo unaoleta nafuu, sabab kuna misimamo inaleta maumivu kwa wengine..huo ni upande mmoja, upande wa pili ni watanzania wenyewe..wangapi wako tayari kuwa kwenye vyama vya upinzani kwa hali na mali? wachache sana..tena kwa vijana hawa wa leo ndio hakuna kabisa! Aina ya watu unahitaji pia aina ya viongozi wanao-match na aina ya watu..upande wa tatu ni dola, iangalie matendo yake inavyofanyia watu na vyama vya upinzani..je kwa hali hiyo ni wangapi wanashawishika kuwa vyama vya upinzani kwa dhati kabisa? Hivyo si sawa kuangalia muda tu, au kumuangalia Mbowe peke yake..tutizame mambo kwa ujumla wake!
Mbowe amefanya makubwa CHADEMA Hilo halina ubishi,

Shida ni kutuaminisha kuwa bila Mbowe, bila utajiri wake, CHADEMA itapotea,

Huo mkwamo na kizuizi hicho lazima tukivuke ikiwa tunataka kujenga Taasisi imara.
 
mbowe anabebeshwa lawama maamuzi yote yanapitishwa na kamati kuu

mbowe hakua rais/amiri jeshi kwamba anatoa maagizo bila kupingwa bali cabinets ilikaa na lissu .akiwepo

kama mnaondoka chadema nyie ondokeni sisi tupo tutapambana had ukamalifu wa dahari
Mkuu umeishajiuliza kwanini watu fulani viganganizi kama kupe kutoondoka Chadema wanayodai Mbowe kaiuwa,wasianzishe SACCOS za kwao au kuhamia vyama vingine? Kwa sababu wanajua hawatatoboa.
Why Mbowe? ooh kakaa sana kwenye uwenyekiti,anzisha chama chako uwe Kiongozi Mkuu kama Zito au wenyekiti wa maisha kama wa Profesa Lipumba au kuunda chama ambacho uongozi ni wa mzunguko kama wa Acient Greece democracy.
Au kimbilia basi CCM ukafunzwe leadership code kama utatoboa.
Waacha chuki binafsi kwa sababu ya kutafuta maslahi binafsi,usione vinaeelea vimeundwa.
 
Alaaa kumbe! Kwa hiyo mumemshawishi Mh. Lissu apige penati, huku hamtaki golikipa awepo golini eeeh?
Mbona, kabla Mh. Lissu hajabadili uamuzi wa kuutaka Uenyekiti, hamkuonyesha kuwa hamumtaki Mh. Mbowe auwanie tena uenyekiti?
Nendeni kumstaafisha kupitia boksi la kura!
Ww ndio unadhani watu hawakumtaka Mbowe hadi Lisu alipotaka kugombea. Mfano mrahisi ni mimi binafsi, baada ya ujio wa Lowassa hadi leo nimekuwa nikisema Mbowe hastahili kuwa mwenyekiti wa cdm tena.
 
Mkuu umeishajiuliza kwanini watu fulani viganganizi kama kupe kutoondoka Chadema wanayodai Mbowe kaiuwa,wasianzishe SACCOS za kwao au kuhamia vyama vingine? Kwa sababu wanajua hawatatoboa.
Why Mbowe? ooh kakaa sana kwenye uwenyekiti,anzisha chama chako uwe Kiongozi Mkuu kama Zito au wenyekiti wa maisha kama wa Profesa Lipumba au kuunda chama ambacho uongozi ni wa mzunguko kama wa Acient Greece democracy.
Au kimbilia basi CCM ukafunzwe leadership code kama utatoboa.
Waacha chuki binafsi kwa sababu ya kutafuta maslahi binafsi,usione vinaeelea vimeundwa.
Kwani hiyo cdm kaanzisha Mbowe?
 
Hv vyama vya upinzani havina ajenda yoyote zaIdi kupiga dili..ndio maana vimepoteza mvuto kwa wananchi…mbowe ametia aibu sana kutaka kugombea…wamefanya vyama ni vyao….angalia mzee lipumba eti nae kashinda uongozi.
Mamako ana ajenda gani mbali na kuuwa watu bwabwa wewe.
 
walikuwepo kina Mtikila na confrotational approach yake..nani alimuunga mkono?
Mbona Dr Slaa aliifanya na tulimuunga mkono. Unadhani after Slaa angekuja Heche kwenye ukatibu au Lissu uenyekiti tungekua second fiddle kwa CCM? We need to radicalize our opposition ndio lugha pekee CCM wanaijua, tukiendelea na diplomacy za Mbowe mwakani wataiba tena majimbo yote.
 
Hellow Tanganyika!!

Uliyoyasikia kuhusu wewe kuchoka Si mwili pekee, Bali Fikra za kuleta uono Mwema wa chama na Nchi chini ya uongozi wako.

1. Kupoteza kumbukumbu ni kiashiria kikuu Cha Mkt Mbowe kuchoka, Ndugu Mbowe umeshasahau kuwa Mwaka 2014 chama chako kimekuwa mstari wa mbele kudai katika mpya na kuheshimu maoni ya wananchi kwamba kuwepo na ukomo wa uongozi katika ngazi zote, watu wastaafu umri ukifika waingie Damu changa na Fikra mpya. Sasa iweje tudai Katiba mpya ilhali iliyopo imeweka ukomo wa Rais kukaa mamlakani wakati CHADEMA hakuna ukomo Kwa nafasi ya mkt wa chama Kwa muda wa uongozi?

2. Ujio wa Lowwassa CHADEMA ulichangia Kwa kiasi kikubwa kuchafua image ya chama mbele ya umma. Haya yote yametokea Ukiwa mkt wa chama.

3. Kuingia na kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024, ni Moja ya mapungufu ya uongozi wako, kushindwa Kwa chama chako ni mapungufu ya uongozi wako, yalitokea mambo hayo hayo chini ya Magu 2019, na kwann hukujifunza ukarudia Yale Yale Yale 2024?

4. Kushindwa Kwa maridhiano uliyokiaminisha chama ni mapungufu Yako binafsi kama kiongozi, uliwaamini vipi CCM na kumsafisafisha mkt yule wa upande wa pili Hadi kumwalika Moshi kwenye sherehe za Bawacha?

5. Kuingia katika maridhiano bila idhini ya chama ni jambo la kutiliwa shaka pia, kwanini hukuomba ruhusa uende kwanza nyumbani, ubadili nguo, Kisha uonane na wanachama na viongozi Kisha yafanyike maamuzi ya kuingia katika meza ya maridhiano na CCM? Kwanini kupiga GIA ya angani Toka gerezani Hadi jumba jeupe?

6. Jitihada zako kukemea RUSHWA ndani ya chama ni za chini sana, matumizi na vipaumbele katika matumizi ya pesa za chama pia ni dhaifu, hayo pia ni mapungufu yanayokuhusu kama Mwenyekiti wa CHADEMA.

Ndugu Mbowe, baba Yako wa Ubatizo Mwl Nyerere aliachia Urais kukiwa hakuna mtu maarufu kumzidi, na alikuwa na nguvu pia na uwezo kifikra kuendelea kuwa Rais wa Nchi.

Ushauri: Jitoe mbele ya safari kipindi Cha compaign au subiri MAPINDUZI Toka Kwa vijana Rika la kina Sativa.

Mungu ibariki CHADEMA.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏
Hoja imeungwa mkono na mimi
 
Back
Top Bottom