Uchaguzi 2020 Mbowe wa COVID-19 sio wa Uchaguzi 2020

Msulibasi

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
5,947
Reaction score
7,939
Inakuwaje mwenyekiti wetu Freeman Alkael Mbowe kuwa baridii kipindi hiki ambacho uenyekiti wake ulipaswa kujidhihiri.

Inakuwaje kila kona watu wa CHADEMA wanaenguliwa kihuni na hakuna reaction ya maana kutoka ngazi ya juu ya chama zaidi ya tweets.

Kumtegemea mgombea urais Lissu ni kujidanganya. Lissu si mkomavu kuweza kusimama Kama mgombea urais na muongozaji zoezi kwa wabunge na madiwani watia nia. Lissu anachojua Nigo urais na Magufuli Basi.

Lissu hajui kule MOROGORO kina Minja Devotha kimewakuta nini. Hata akijua Lissu udiwani, Ubunge si mkazo.

Mbowe toka haraka kaa na viongozi wakuu wenzio wa vyama muone nini kifanyike.

Kadiri manvyositasita na kuzubaa ndivyo mnavyowapa nguvu wahuni kuwaondoa kwenye reli. Hali ikishazidi kuwa mbaya kwa wagombea udiwani na ubunge basi wananchi watapoteza Ari na CCM itafikia lengo la kuwa na wabunge wa CCM pekee bungeni. Mbatia viti maalum vya Rais.

Niwaambie tena nia ya kuufuta upinzani ipo palepale. Upinzani sio wananchi km mnavyojidanganya. Kuufuta upinzani ni kufuta wawakilishi wa wananchi.

Muwe makini , CCM mpya bado Ina lengo la kumwongezea Magufuli mihula.
 
CDM walishapotezana mapema sana, hata kuwahudumia tu waandishi wa habari ili wawe sehemu ya msafara wa Lissu wameshindwa, saivi wanasubiria huruma ya AyoTv , hata a Diamond anawashinda, useless kabisa hawa...
 
'Eti Mbowe wa Covid 19' ...! Ule upuuzi wa kuwaamrisha wenzie kujilock down halafu anawarusha tena mule mule mjengoni baada ya wiki 2 ulikuwa wa kiwango cha SGR.
 
Mlamu usiwe mjinga, sheria ya uchaguzi inasema nini kuhusu pingamizi... anaweka mgombea au mwenyekiti wa chama?
 
Wajinga kama nyie ndio mbowe anajivunia sana kuwa na wanachama kama wewe!

Ninyi ndo mtaji wa mbogamboga Lumumba, mmeshikiwa akili (sidhani kama mlikuwa nazo hata hivyo) hizo ndogo kama misukule... hamuwezi kufikiri kwa ajili yenu!
 
Hivi upinzani nao huwa wanakoselewa au kushauriwa? hawa jamaa muda wote wako sahihi kwa kila jambo.
 
Mbowe kisha maliza pesa zote na anashindwa kuinasua akaunti yake ktk mtego wa wizi alioufanya. Anahangikia jimbo la hai, akirudi utamsikia anajidai ana maslahi ya taifa.
 
Mwenyekiti na katibu mkuu wafanye kazi yao.
Makamu Mwenyekiti keshawafunika..na subiri baada ya MDA mchache watapoteana sana pale Ufipa...Lissu ni lazima awe Rais au Chairman..less than that Patachimbika.
 
Mbowe wakati mwengine anajielewa, hawezi kufanyakazi na Lissu huyu wa ubeligiji. Kwanza Lissu anajifanya mjuaji, ni mropokaji vilivyo, tamaa ya cheo, hawezi uongozi wa kushirikisha wengine au kukasimu/deligate majukumu, ni yeye tu anayetaka kila fursa ya kuwa mbele ya kamera, ana mkubali Mbowe kinafiki tu wakati moyoni mwake angetaka awe mgombea na mkt wa cdm na yuko njiani kufikia ndoto hiyo.

Lakini kwa mwanasiasa anayejielewa na mwenye malengo makubwa ya kisiasa ya mbeleni, hili na washauri wana siasa waliojipambanua na wanao chipukia. Kumshabikia Lissu, kumshabikia, kumdhabikia na kuambatana naye ni kujinajisi kisiasa. Utaishia kudharaulika kwa Watanzania baada ya muda si mrefu ujao.
 
CDM walishapotezana mapema sana, hata kuwahudumia tu waandishi wa habari ili wawe sehemu ya msafara wa Lissu wameshindwa, saivi wanasubiria huruma ya AyoTv , hata a Diamond anawashinda, useless kabisa hawa...
Mtu makini kwenye profession yoyote iwe ni uandishi wa habari, muziki na kadhalika huwezi kujihusisha na chadema katika kilindi hiki...
 
'Eti Mbowe wa Covid 19' ...! Ule upuuzi wa kuwaamrisha wenzie kujilock down halafu anawarusha tena mule mule mjengoni baada ya wiki 2 ulikuwa wa kiwango cha SGR.
Alikua very active kwa issue za subira. Sasa hizi issue zenye ulazima wa kutoa povu hayupo
 
Mlamu usiwe mjinga, sheria ya uchaguzi inasema nini kuhusu pingamizi... anaweka mgombea au mwenyekiti wa chama?
Pingamizi sio ishu katika siasa Kuna mengi . Unaweka mapingamizi na unaweka pressure . Sasa mkoa wa MOROGORO aslimia 70 ubunge na udiwani mmeondolewa , na hata hizo rufaa hawazipokei.


Nimedurahishwa na kina mama wa Myama ACT kwa kwenda halmashauri kwa maelfu kupinga dhuluma. ACT wapo shapu kiasi bahati mbaya chama Chao kidogo
 

Sasa hao kina mama ndo mwenyekiti!! Mbona kwa CHADEMA umemhusisha Mbowe?

Kuenguliwa kwa wagombea ni figisu za tume zenye baraka kutoka kwenye mamlaka kandamizi iliyopo kwa sasa.
 
Hivi upinzani nao huwa wanakoselewa au kushauriwa? hawa jamaa muda wote wako sahihi kwa kila jambo.
Tunajaribu kuwatoa usingizini hawaelewi , CCM imedhamiria kutokuwa na mbunge wa upinzani October. Hata huyo Mbowe atakuja jikuta anafanyiwa uhuni na hatakuwa mbunge. Nawashauri kabla wananchi hawajakata tamaa viongozi wa upinzani wakutane na kuweka shinokizo kubwa kwa namna watakayoona.


Lisu ametumia nguvu kubwa kwa Magufuli na kusahau kuwa Kama majimbo yakienda CCM na kata zote hata ufanyaje mgombea urais utaambulia zero point percentage
 
Sasa hao kina mama ndo mwenyekiti!! Mbona kwa CHADEMA umemhusisha Mbowe?

Kuenguliwa kwa wagombea ni figisu za tume zenye baraka kutoka kwenye mamlaka kandamizi iliyopo kwa sasa.
Kina mama wale Ni matokeo ya pressure ya viongozi wa ACT na mgombea wao wa urais ingawa nao walichelewa sana kuchukua hatua za nguvu na mengi yakatokea.

Dalili za uhuni Lindi zilianza na sababu ni ujakika wa kushindwa vibaya. Sio Siri Lindi na kusini Wana jambo lao Ila CCM wamewawahi .Hii so strategy ya wagombea wa CCM Ni strategy ya chama kwa maeneo magumu.

MOROGORO wameonesha muamko na hii imewatisha sana CCM kwamba MOROGORO ya Leo sio Ile ya kale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…