The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Viongozi wa Taasisi za Elimu wakiwemo Wakuu wa Shule, wilayani Mbozi, wametakiwa kuwa wabunifu wa miradi ya kimaendeleo, katika maeneo yao ya shule, hali ambayo itawasiaidia wanafunzi kujifunza stadi za maisha pamoja na kuwapatia kipato ambacho kitasaidia kuendesha shughuli za shule ikiwemo kukidhi baadhi ya mahitaji kwa walimu na wanafunzi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Bw. Hamad Mbega, alipokuwa katika shule ya sekondari Ndugu, iliyopo Kata ya Hasamba, wilayani humo baada ya kutembelea miradi ya shule hiyo ikiwemo, ufugaji wa ng’ombe kwa ajili ya maziwa na uzalishaji wa nishati mbadala wa biogas, ufugaji wa samaki, kilimo cha mbogamboga, uchimbaji wa kisima kikubwa cha maji, kilimo cha zao la kahawa pamoja na mradi wa mashine ya kusaga na kukoboa.
Bw. Mbega ameupongeza uongozi wa shule hiyo kwa ubunifu huo nakuzitaka taasisi zingine za elimu kuiga ubunifu huo huku mkuu wa shule hiyo yenye wanafunzi 934 bwana cosmas nzowa akisema lengo la miradi hiyo ni kuimarisha lishe kwa walimu na wanafunzi sambamba na kuboresha uhusiano na jamii inayozunguka eneo la shule hiyo.