Mbunge adai Masasi hawana shida ya vitabu shuleni

kiduchu

Member
Joined
Feb 25, 2008
Posts
42
Reaction score
19
Katika hali isiyo ya kawaida Mbunge wa Masaai amewashambulia wanaodhaniwa kuwa ni watia nia. Mbunge huyo amedai kuwa watu wastaafu hawapaswi kugombea ubunge. Akiongea katika mkutano na wananchi amedai kuwa mbunge anatakiwa awe kijana mwenye kuweza kukimbia kimbia, hivyo yeye ndio anafaa. Aidha amejinasi kuwa Masasi hakuna shule yenye shida ya vitabu na DED anashangaa mtu kuleta msaada wa vitabu kwenye jimbo lake.
Hivi ni kweli DED atakuwa hajui shida ya vitabu kwenye halmashauri ya Masasi? Au amejitoa ufahamu ili kumbeba huyu mtukanaji!! Basi hivyo vitabu tuleteeni sisi huku Songea.
 
Attachments

  • 5a385eba-9e76-495b-846b-dde33da4cc07.mov
    21.6 MB
Mtu yuko radhi watoto wakose vitabu kwa sababu ya kutetea Ubunge wake?

Huyo Mbunge kuwa kwenye hiyo nafasi inamaanisha hili Taifa lina utitiri wa vilaza kupita maelezo.

Kuna mambo yanaumiza sana.
 
Katika hali isiyo ya kawaida Mbunge wa Masaai amewashambulia wanaodhaniwa kuwa ni watia nia. Mbunge huyo amedai kuwa watu wastaafu hawapaswi kugombea ubunge. Akiongea katika mkutano na wananchi amedai kuwa mbunge anatakiwa awe kijana mwenye kuweza kukimbia kimbia, hivyo yeye ndio anafaa. Aidha amejinasi kuwa Masasi hakuna shule yenye shida ya vitabu na DED anashangaa mtu kuleta msaada wa vitabu kwenye jimbo lake.
Hivi ni kweli DED atakuwa hajui shida ya vitabu kwenye halmashauri ya Masasi? Au amejitoa ufahamu ili kumbeba huyu mtukanaji!! Basi hivyo vitabu tuleteeni sisi huku Songea.
Pesa kubwa wanazokula huko bungeni zinawapa upofu ili wang'ang'anie Bila hata kujali shida za wananchi wanao wawakilisha !
 
Ndio mjue tuna vilaza huko Bungeni. Kama vitabu ni jambo la kijinga na kipuuzi huko Masasi, utashangaa vipi mkoa wa Mtwara kuwa nyuma kielimu? Na DED Jichabu anabariki. Poleni Masasi, maana Mbunge na DED lao moja.
 
Bado nitamlaani sana ******** kwa Kuhalalisha hii dhambi ya kupita bila kupingwa haya yote ni matokeo ya dhambi zake Mungu alizomuadhibu Vikali.

Hebu fikiria kweli Mbunge kwanza anaongea kwa kutetemeka hivi unadhani hata kutoboa atatoboa kura zikisimamiwa vizuri? Yani Hana uwezo wowote wa kujenga hoja alafu ndio CCM wanasema anawakilisha wananchi
 
...Aidha amejinasi kuwa Masasi hakuna shule yenye shida ya vitabu na DED anashangaa mtu kuleta msaada wa vitabu kwenye jimbo lake.
Hivi ni kweli DED atakuwa hajui shida ya vitabu kwenye halmashauri ya Masasi? Au amejitoa ufahamu ili kumbeba huyu mtukanaji!! Basi hivyo vitabu tuleteeni sisi huku Songea.
Umeunganisha sentensi kiasi kwamba si rahisi kwa wasomaji kujua ipi ni kauli ya mbunge na ipi ni 'my take yako'.
 
Katika hali isiyo ya kawaida Mbunge wa Masaai amewashambulia wanaodhaniwa kuwa ni watia nia. Mbunge huyo amedai kuwa watu wastaafu hawapaswi kugombea ubunge. Akiongea katika mkutano na wananchi amedai kuwa mbunge anatakiwa awe kijana mwenye kuweza kukimbia kimbia, hivyo yeye ndio anafaa. Aidha amejinasi kuwa Masasi hakuna shule yenye shida ya vitabu na DED anashangaa mtu kuleta msaada wa vitabu kwenye jimbo lake.
Hivi ni kweli DED atakuwa hajui shida ya vitabu kwenye halmashauri ya Masasi? Au amejitoa ufahamu ili kumbeba huyu mtukanaji!! Basi hivyo vitabu tuleteeni sisi huku Songea.
Inawezekana kweli vitabu havihitajiki kwani hata vinavyokuwepo wanafunzi huwa hawavitumii.
Nilishuhudia wakati fulani vitabu vikiwa vimezagaq hovyo vikiwa vinatafunwa na mchwa na panya kwenye shule mbalimbali za wilaya ya Masasi.
 
Vita ya ubunge imekuwa kubwa Sana....Huyu jamaa alikuwa vizuri Sana kipindi yupo pale NIC sijui amepatwa na wazimu gani Hadi kuwa mjinga kiasi hiki
 
Katika hali isiyo ya kawaida Mbunge wa Masaai amewashambulia wanaodhaniwa kuwa ni watia nia. Mbunge huyo amedai kuwa watu wastaafu hawapaswi kugombea ubunge. Akiongea katika mkutano na wananchi amedai kuwa mbunge anatakiwa awe kijana mwenye kuweza kukimbia kimbia, hivyo yeye ndio anafaa. Aidha amejinasi kuwa Masasi hakuna shule yenye shida ya vitabu na DED anashangaa mtu kuleta msaada wa vitabu kwenye jimbo lake.
Hivi ni kweli DED atakuwa hajui shida ya vitabu kwenye halmashauri ya Masasi? Au amejitoa ufahamu ili kumbeba huyu mtukanaji!! Basi hivyo vitabu tuleteeni sisi huku Songea.
Shida ya vitabu ipo nchi nzima. Inatakiwa iwe mtoto mmoja, kitabu kimoja. Huko Masasi hali ipo hivyo?

Mbunge pokea msaada wa vitabu. Kama unataka mchezeshee fitina huyo mleta msaada wa vitabu unachomekea vitabu vya ushoga ili vikamatwe na achufuke. Si ndiyo siasa zenu za maji taka!
 
Back
Top Bottom