Mbunge adai SGR itajengwa kwa miaka 81

Mbunge adai SGR itajengwa kwa miaka 81

Trust None

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
1,260
Reaction score
4,419
Mbunge wa Handeni Mjini CCM, Reuben Kwagilwa, ameishauri Wizara ya Fedha na Mipango, waangalie namna ya kufadhili miradi mikubwa kwa mfumo wa dhamana ya miundombinu ‘infrastructure bond’ ili kuiwezesha Serikali kutoa huduma za wananchi kila siku.

Amesema isipofanya hivyo mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa wa SGR utachukua miaka 81 kukamilika kwakuwa mpaka sasa hata kilometa 300 bado hazijakamilika.

Kwagilwa ametoa ushauri huo Ijumaa Aprili 9, 2021 bungeni wakati akichangia mjadala wa mpango wa tatu wa maendeleo wa kitaifa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2021/22 - 2025/26,

“Standard Gage Railway tunayoijenga ukijumlisha zile njia tunazotakiwa kujenga ni kilomita 4886 hapo naongelea zile njia tu, siongelei mahala ambapo reli huwa zinapishana. mpaka sasa tumeshajenga kipande kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kilometa 300 na tunaendelea kipande cha Morogoro Makutupora kilometa 422 lakini tuko upande mwingine wa Isaka na Mwanza kilometa kilometa 249

Kwa namna tunavyohudumia mradi huo kama tukiendelea kwa mfumo huo tutajenga kwa miaka 81 kwa nchi nzima ikiwa miaka mitano tumejenga kwa kilameta 300 na kilometa zilizosalia tutazijenga kwa miaka 81 hii katika nchi ambayo inapambana kujenga uchumi kasi hiyo haikubaliki na imegharimu Sh11 trilioni ambazo ni ‘hido investiment’ kwa sababu hatutaanza kutumia leo.,”amesema

Ameongeza “Serikali inatakiwa kujifunza na kuondokana na mfumo wa kizamani wa kufadhili miradi mikubwa kwa sababu inajipa pressure kubwa halafu inashindwa kupeleka huduma za kila siku kwa wananchi wake” amesema.

Chanzo: Mwananchi.
 
Tril 11 ni sawa sawa na double highways za
Dar Arusha 1T

Dar Mbeya 2T
Dar Mwanza 2T
Dar Mtawara 1T
Na barabarara zote za kuingia miji mikubwa na stand zake za kisasa pamoja na hospitali 2 zenye hadhi ya Nairobi Hospital

Miradi ya Reli ni pasua kichwa kwenye nchi ambayo bado asilimia 90 ya shule za kata hazina maabara na hospitali zisizo na vifala vya kisasa.

Sijawah kuikubali miradi ya huyu Bwana.
 
Hii serikali ya huyu mama sidhani kama itakamilisha hii miradi kama pasipokuwepo na juhudi za dhati, wanatakiwa wajue wapi watapata pesa za kukamilisha, labda wachina waingilie kati wakamilishe then wauendeshe huo mradi kwa miaka kadhaa, kinyume na hapo kazi ipo.

Hii SGR itatukamua haswa, it's a challenge they must face, no way back, ikibidi marupurupu ya wabunge yafyekelewe mbali na mishahara yao ipunguzwe pesa iende huko.
 
Back
Top Bottom