Mbunge adai SGR itajengwa kwa miaka 81

Mbunge adai SGR itajengwa kwa miaka 81

Watafute mbinu na namna ya kuumaliza...kuuacha si hasara mara mia?
 
R.I.P JPM;VIJANA TULIODHANI WATAKUTETEA TUNAONA WAKIUNGANA KUPOTEZA MEMA ULIYOYAFANYA
Anayetegemea akili yake hupotea na anayetegemea mali yake hupungua, anayetegemea watu nao huchoka lakini anayetegemea Mungu hufanikiwa.
 
Hapana
Kama SGR iishie hapo Moro
HEP wafanye kias wazalishe umeme mdogo ... otherwise hizo drama hazitaisha isha leo
Kuishia Moro tutakuwa tunalenga nini Moro kitakachoturudishia angalau robo gharama? Na hicho kipande kilichojengwa mbele je? Wakiingia wa mkopo nao watatushughulisha mpaka vitukuu watabeba mzigo..Mbona kazi tunayo...

Sorry, HEP ni?
 
Kuishia Moro tutakuwa tunalenga nini Moro kitakachoturudishia angalau robo gharama? Na hicho kipande kilichojengwa mbele je? Wakiingia wa mkopo nao watatushughulisha mpaka vitukuu watabeba mzigo..Mbona kazi tunayo...

Sorry, HEP ni?
Huo mradi hata ukikamilika hautakaa ulipe boss .. na ndio maana Ndungai alipendekeza PPP waingie ubia na kampuni binafsi kwenye uendeshaji
HEP ni Hydro Electric power
 
Tril 11 ni sawa sawa na double highways za
Dar Arusha 1T

Dar Mbeya 2T
Dar Mwanza 2T
Dar Mtawara 1T
Na barabarara zote za kuingia miji mikubwa na stand zake za kisasa pamoja na hospitali 2 zenye hadhi ya Nairobi Hospital

Miradi ya Reli ni pasua kichwa kwenye nchi ambayo bado salimia 90 ya shule za kata hazina maabara na hospitali zisizo na vifala vya kisasa...
Sijawah kuikubali miradi ya huyu Bwana.
Kwa hapa ninaweza kupishana na wewe kidogo kiongozi, mimi nadhani swala zima nivipaumbele.

Kuna mwengine anaweza kuwa na 10m akafikiria kununua gari afanye daladala mjini apate pesa, mwengine atafungua duka auze bidhaa, wengine atafungua mpesa mwengine atafikiria akafanye investment shambani lakini yote ya yote; kila mmoja anaangalia faida iwe ni long run au short run investment
 
Kwa hapa ninaweza kupishana na wewe kidogo kiongozi, mimi nadhani swala zima nivipaumbele.

Kuna mwengine anaweza kuwa na 10m akafikiria kununua gari afanye daladala mjini apate pesa, mwengine atafungua duka auze bidhaa, wengine atafungua mpesa mwengine atafikiria akafanye investment shambani lakini yote ya yote; kila mmoja anaangalia faida iwe ni long run au short run investment
Mkuu upo sawa, kwenye Economics inaitwa opportunity costs.
Na mtazamo wangu ni kwamba faida ya huo mradi ni ndogo mno ukilinganisha na vipaumbele nilivyovitaja..
Kumbuka tayar tuna NG Mtwara, kwanini tusi capitalize huko.
Yes pengine kuna mikataba ya kimangungo mbona wa Accacia tulipindua.. so inawezekana
 
Tril 11 ni sawa sawa na double highways za
Dar Arusha 1T

Dar Mbeya 2T
Dar Mwanza 2T
Dar Mtawara 1T
Na barabarara zote za kuingia miji mikubwa na stand zake za kisasa pamoja na hospitali 2 zenye hadhi ya Nairobi Hospital

Miradi ya Reli ni pasua kichwa kwenye nchi ambayo bado salimia 90 ya shule za kata hazina maabara na hospitali zisizo na vifala vya kisasa...
Sijawah kuikubali miradi ya huyu Bwana.
Wapika kelele hawawezi kukuelewa
 
Hii serikali ya huyu mama sidhani kama itakamilisha hii miradi kama pasipokuwepo na juhudi za dhati, wanatakiwa wajue wapi watapata pesa za kukamilisha, labda wachina waingilie kati wakamilishe then wauendeshe huo mradi kwa miaka kadhaa, kinyume na hapo kazi ipo, hii SGR itatukamua haswa, it's a challenge they must face, no way back, ikibidi marupurupu ya wabunge yafyekelewe mbali na mishahara yao ipunguzwe pesa iende huko.
Tuliambia pesa zipoo!! nyuma mikamera,kumbe zinapigwa
 
Tril 11 ni sawa sawa na double highways za
Dar Arusha 1T

Dar Mbeya 2T
Dar Mwanza 2T
Dar Mtawara 1T
Na barabarara zote za kuingia miji mikubwa na stand zake za kisasa pamoja na hospitali 2 zenye hadhi ya Nairobi Hospital

Miradi ya Reli ni pasua kichwa kwenye nchi ambayo bado salimia 90 ya shule za kata hazina maabara na hospitali zisizo na vifala vya kisasa...
Sijawah kuikubali miradi ya huyu Bwana.
Viongozi wa sasa wana hali ngumu sana jinsi ya kuwaelezea wananchi ugumu wa hii miradi na wakaelewa,ni miradi migumu kwelikweli.mimi nilitamani marehemu angekuwepo ili apambane mwenyewe na hii miradi na hali tuliyokuwa tunaenda nayo kusingekuwa na nafuu ya maisha kwa mwananchi hata kidogo kwa zaidi ya miaka 20 ijayo hilo ndilo lililokuwa linaniogopesha,sikupenda tufike huko kabisa lakini nilitamani washangiliaji waje waisome namba na tungeisoma kwelikweli,baada ya kubanwa hasa wafanyabiashara,matajiri,wafanyakazi hali ilikuwa inaanza kuhamia kwa wananchi,mambo kama kitambulisho cha machinga,parking charges zile za tarura sijui zilishatoka huko mijini zikaingia mitaani kabisa,trafiki wakaingia mitaani kwenye parking kukagua magari yanayodaiwa faini,zile kodi za kumiliki kisima cha maji,gharama za kumiliki youtube chaneli,gharama za kumiliki drone,kodi za kufanya sherehe kwenye ukumbi zilianza,kiufupi kungekuja tozo mbalimbali ambazo kiujumla wake zingembana mwananchi wa hali ya chini na hali hiyo ingechukua muda mrefu maana ni mpaka hii miradi mikubwa iishe ndo nafuu ingepatikana.
 
Lakini haya wakiyasema wapinzani,au nao ccm wameamua kujipinzani?

Inaonekana humo ndani m'binyo wake ulikuwa siyo mchezo nahisi hata walipokuwa kwenye vikao na boss wao mtu akijisikia kwenda haja alikuwa anaomba ruhusa kwanza ila ndo mjifunze madhara ya kukabidhi madaraka kwa wafugaji.
 


Ujenzi reli ya TAZARA funzo chanya kwa mradi wa SGR​

February 21, 2019

HILAL K SUED
Wakati serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli ikiwa mbioni kufanikisha mradi kabambe wa kujenga reli mpya ya kisasa ya Standard Gauge (SGR) kati ya Dar es Salaam kwenda Bara ambayo itachukua nafasi ya ile ya zamani iliyojengwa na wakoloni wa Ujerumani zaidi ya karne moja iliyopita, ni vyema tukajikumbusha reli nyingine iliyojengwa katika mradi mwingine kabambe zaidi enzi hizo – zaidi ya miaka 40 iliyopita.

Hii ni Reli ya TAZARA inayomilikiwa kipamoja kati ya Tanzania na Zambia. Hivyo wakati tunaendelea na mradi huu wa sasa ni vyema ule wa zamani ukatupa somo la historia la kujifunza – na hivyo kutilia maanani jambo muhimu kabisa kwamba kujenga reli na kuiendesha ni masuala mawili yaliyo tofauti kabisa.

Kwani hakuna aliyewaza kwamba TAZARA, inayomilikiwa kipamoja baina ya Tanzania na Zambia baadaye ingejikuta katika hali ya kupumulia mashine na kuendesha shughuli zake kutokana na misaada ya kifedha na kiufundi kutoka China – nchi iliyoijenga reli hiyo katika miaka ya 70.

Na kuhusu Reli ya Kati – kuna wanaohoji iwapo tulishindwa kuiendesha reli hiyo ambayo tulikabidhiwa na wakoloni kwenye sahani ya fedha, tungepata wapi utaalamu wa kuendesha reli nyingine mpya? Na tayari tuna somo la kujifunza hapa kuhusu ule ukodishaji ulikouwa na utata mkubwa wa shirika la reli TRC kwa RITES karibu miaka 10 iliyopita.
RITES walishindwa kuliendesha shirika letu la reli na waliondoka baada ya kutia hasara kubwa kwa wananchi.

Na iwapo habari kamili ya yaliyojiri katika mkataba baina ya TRC na RITES utaanikwa hadharani, zitaonyesha ilikuwa kashfa inayoweza kuzishinda kashfa zote zilizowahi kutokea na kuiathiri nchi hii masikini kiuchumi katika miaka ya karibunui.

Reli ya TAZARA, ambayo pia huitwa Reli ya Uhuru (Uhuru Railway) ilijengwa kati ya 1970 na 1975 kwa lengo la kuipa nchi ya Zambia iliyokuwa haina pwani ya bahari ‘kiunganisho’ hadi Bandari ya Dar es Salaam kama njia mbadala ya kusafirisha bidhaa zake zilizokuwa zikipitia Rhodesia (sasa Zimbabwe), Afrika ya Kusini na Msumbiji.

Ikumbukwe nchi hizo tajwa zilikuwa bado chini ya utawala wa kikoloni na/au Wazungu wachache huku mapambano ya kudai uhuru yakiendelea. Kwa upande wa Tanzania lengo lilikuwa ni kusukuma maendeleo katika maeneo reli hiyo ingepita.

Hivyo mradi huu tayari ulikuwa na soko kuhusu matumizi yake (turnkey project) na uliwezeshwa na kugharamiwa na fedha kutoka Jamhuri ya Watu wa China. Jumla ya gharama ilikuwa Dola za Kimarekani 500 milioni (wakati ule), na hivyo kuufanya mradi huo kuwa ni mkubwa zaidi kuliko miradi yote ya China kwa nchi za nje – wakati ule.

PINGAMIZI ZILIZOJITOKEZA DHIDI YA MRADI
Baada ya Vita vya Kwanza ya Dunia, nchi hii, wakati huo ikiitwa German East Afrika ilikabidhiwa Uingereza kuitawala chini ya Udhamini ya iliyokuwa Jumuiya ya Kimataifa (League of Nations – mtangulizi wa Umoja wa Mataifa (United Nations). Tangu enzi hizo, mipango wa kujenga njia ya reli ilikuwa inafikiriwa kuunganisha Tanganyika na iliyokuwa Rhodesia ya Kaskazini (sasa Zambia).

Hata hivyo, mipango hiyo ilikaa ndani ya makabati tu kutokana na kudorora kwa hali ya uchumi duniani katika miaka ya 1930. Baada ya Vita ya Pili ya Dunia (1939-45) wazo la kutandika reli hiyo liliibuka tena.

Mwezi Aprili 1949 ramani iliyochapishwa katika Gazeti rasmi la Reli (Railway Gazette) ilionyesha mchoro wa njia ya reli kuanzia Dar es Salaam hadi Kapiri Mposhi, Zambia na haikuwa mbali sana na njia ambayo miaka 20 baadaye ilianza kujengwa kwa msaada wa Wachina.

Na Ripoti ya 1952 ya Sir Alexander Gibb na wenzake ilisema kwamba reli kati ya Rhodesia na Tanganyika isingekuwa na tija yoyote kiuchumi kutokana na kiwango kidogo cha maendeleo ya kilimo katika maeneo itakayopita na kwamba reli zilizopo kutoka Rhodesia kupitia Msumbiji na Angola zinatosha kwa ajili ya kusafirisha madini ya shaba ya Zambia kwenda nje.

Vile vile Ripoti ya Benki Kuu ya Dunia ya 1964 nayo pia ilihitimisha kwamba reli kati ya Zambia na Tanzania haikuwa na tija kiuchumi, na ikapendekeza badala yake ijengwe barabara.

Wazo la kujenga reli kati ya Zambia na Tanzania lilipata msukumo mpya mwaka mmoja baada ya uhuru wa Zambia pale, mwaka 1965 utawala wa Wazungu wachache wa Rhodesia chini ya mlowezi Ian Smith kujitangazia uhuru kutoka Uingereza (Unilateral Declaration of Independence – UDI) na hivyo kuhatarisha njia za kibiashara za Zambia.

Ndipo Rais Julius Nyerere na mwenzake wa Zambia Kenneth Kaunda walianza kufuatilia njia nyinginezo kujenga reli mbadala. Nyerere baada ya kutembelea China alipewa timu ya wapimaji wa ardhi ambao Oktoba 1966 walitoa ripoti yao fupi.

KAZI MUHIMU ALIYOFANYA ABDULRAHMAN BABU
Hata hivyo Kaunda hakuwa na imani sana kuwahusisha Wakomunisti (utawala wa China) na aliona nchi za magharibi ndiyo zingefaa zaidi katika kazi hiyo.
Hivyo uchunguzi wa anga uliofanywa na timu iliyojumuisha Waingereza na Wacanada ilitoa ripoti nzuri Julai 1966, lakini ahadi ya fedha za kugharamia mradi kutoka nchi hizo haikutolewa.

Tangu awali kiongozi wa China, Mwenyekito Mao Zedong alikuwa tayari kutoa fedha, wakati ile ilikadiriwa kuwa Dola za Kimarekani bilioni moja ili kujiongezea kura dhidi ya Urusi ya Kisovieti katika Mkutano wa Wakuu wa nchi za Asia na Afrika uliokuwa unafanyika Algiers mwaka 1966.

Hivyo baada ya kutembelea China Januari 1967, Rais Kaunda alilegeza upinzani wake dhidi ya kuihusisha China katika mradi huo wa reli. Aliyekuwa Wazri wa Biashara na Uchumi katika serikali ya Muungano, Abdulrahman Mohamed Babu alifanya kazi kubwa katika kufanikisha upatikanaji wa fedha kutoka China kwa ajili ya ujenzi wa reli hiyo.

Kutokana na kumbukumbu za kuaminika Nyerere alikuwa anataka kujenga uhusiano wa karibu kati ya Zanzibar na China kwa faida ya nchi nzima (Jamhuri ya Muungano). Hivyo Abdulrahman Babu, aliteuliwa kuwa kiongozi wa ujumbe wa kibiashara ambao ulitangulia ziara ya Nyerere kwenda China.

Matokeo ya ziara hii ni makubaliano ya kibiashara ya Pauni za Kiingereza milioni tano kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitano. Fedha hizi ni mbali na zile Pauni za Uingereza 11 milioni za misaada ya kawaida.

Chini ya makubaliano haya Tanzania itakuwa inanunua kutoka China chochote kile wanachohitaji, nayo China itanunua kutoka Tanzania bidhaa za thamani ya Pauni milioni tano kila mwaka.
Kutokana na uzoefu wake na Wachina na imani yake ya kiitikadi katika namna ya maendeleo yao, Babu alikuwa mtu stahiki kwa kazi hiyo. Aliwaeleza Wachina ugumu ulikuwapo kwa Tanzania kupata fedha za kugharamia mradi wa reli.

CHINA YAKUBALI KUGHARAMIA UJENZI
Tarehe 1 Julai 1965 Serikali ya China ilitoa ahadi madhubuti kwa serikali za Tanzania na Zambia ya msaada wa Pauni za Kiingereza 150 milioni kugharamia reli hiyo.

Septemba 6 1967 Makubaliano yalitiwa sahihi huko Beijing baina ya mataifa matatu – China, Tanzania na Zambia. China ilijitolea yenyewe kujenga reli hiyo katika mkopo wa bila riba utakaolipwa katika kipindi cha miaka 30 kuanzia 1983.

Ujenzi ulianza mwaka 1970 na usafiri rasmi wa reli hiyo ulianza baada ya miaka sita. Reli ilianzia bandari ya Dar es Salaam na kupitia ardhi ya Tanzania kufuata mwelekeo wa kusini-magharibi. Reli hiyo ilipita katika maeneo mengi yasiyokuwa na makazi ya watu.

Tangu reli hiyo ianze kazi kumakuwepo maendeleo ya viwanda katika maeneo ilikopitia, pamoja na mtambo wa uzalishaji umeme wa Kidatu na kiwanda cha karatasi cha Mufindi.

Reli inapishana na barabara kuu ya kwenda Zambia karibu na mji mdogo wa Makambako na inakwenda sambamba nayo hadi Mbeya na mpakani mwa Zambia na inaingia Zambia na kuunganishwa na mfumo wa reli wa Zambia pale Kapiri Mposhi.

UBUNIFU MKUBWA SANA WA UHANDISI TANGU VITA YA PILI
Jumla ya urefu wake ni kilomita 1,863 (maili 1,160) na inaishia ikiwa mita 1,400 juu ya usawa wa bahari. Upande wa Tanzania urefu wa reli hiyo ni kilomita 969, na Zambia ni kilomita 894. Reli hii ilikuwa inatajwa kuwa ni ubunifu mkubwa sana wa uhandisi hapa duniani tangu Vita ya Pili ya Dunia. Ilichukua miaka mitano tu kuijenga na ilimalizika kabla ya muda uliopangwa, mwaka 1975.

Upana wa reli ni mita 1.067 (futi tatu na inchi sita) upana ambao ni sambamba na mfumo wa reli wa Zambia na nchi zingine za Afrika ya Kusini ambayo huitwa Cape Gauge. Reli yetu ya Kati ina upana wa mita moja. Kituo cha kubadili mifumo hii miwili inayohusisha magurudumu kilijenga Kidatu mwaka 1998.

Mbali na upana wake, reli ya TAZARA ilichukua mfumo wa reli nchini China katika miaka ya 70 – hasa katika viunganisho vya mabehewa (couplings), mfumo wa breki, uzito wa mizigo kwenye magurudumu (axle loading – tani 20), aina ya chuma cha reli (high manganese steel) na mataruma (sleepers).

Mataruma ni ya zege zenye nondo ndani kwa reli nzima isipokuwa kwenye madaraja na maungio ambako mbao ndiyo ilitumika.

CHANGAMOTO ZA KAZI YA UTANDIKAJI RELI
Kabla ya kuanza kujengwa wapima ardhi 12 wa kutoka China walitembea kwa miguu kwa miezi tisa kati ya Dar es Salaam na Mbeya ili kubaini njia ambayo reli ingepita.
Baada ya hapo Watanzania wapatao 50,000 na Wachina 25,000 walihusishwa katika kazi ya ujenzi wa reli hiyo ya kihistoria. Katika jua, mvua na upepo vibarua hao waliweza kutandika reli kupitia moja ya sehemu zenye milima mingi zaidi na mabonde Barani Afrika.

Kazi hiyo ilihitaji kusafirisha tani 330,000 za reli ya chuma cha pua na ujenzi wa madaraja 300, mahandaki 23 ya chini kwa chini (tunnels) vituo vya treni (stations) 147.

Nguzo za kushikilia daraja la kuvukia Mto Mpanga zina urefu wa mita 49 kutoka chini na handaki (tunnel) la Irangi lilikuwa na urefu wa kilomita 1.5 ndani ya mlima. Sehemu kati ya Mlimba na Makambako ndiyo ilikuwa sehemu ngumu sana kupitisha reli, kwani ilikuwa ina milima mingi na mabonde ya kina kirefu na pia kuwa katika eneo la mvua nyingi. Mifumo madhubuti ya uondoshaji wa maji ya mvua ililazimika kujengwa.

Asilimia 30 ya madaraja yote, mahandaki na mitaro ya kuondoshea maji, pamoja na upasuaji mkubwa wa majabali ulikuwa katika kipande hiki kigumu cha urefu wa kilomita 16 tu.

Kambi za ujenzi ziliwekwa kila baada ya kilomita 64 na zilikwa zinahamishiwa mbele jinsi kazi ya utandikaji reli ulivyokuwa ikiendelea. Mipapai na migomba ilikuwa inaoteshwa kwenye kambi hizo kwa ajili ya kujipatia chakula kwa vibarua ambao baadhi yao pia walilima bustani za mboga nyakati zisizo za kazi.

MANDHARI YA MAENEO RELI INAKOPITA
Kuanzia Dar es Salaam reli hiyo ilipitia uwanda wa pwani kabla ya kuingia Hifadhi ya Mikumi na ile kubwa ya Selous kwa upande wa kaskazini. Wasafiri wa reli hiyo hupata nafasi ya kuangalia aina mbali mbali za wanyamapori katika Hifadhi ya Selous – kama vile twiga, tembo, pundamilia, swala na kadhalika, na baada ya miaka mingi wamekuja kuzoea na kuvumilia mingurumo ya treni zinapopita.

Baada ya Hifadi ya Selous, reli inapita Bonde la Kilombero lenye rutuba nyingi kwa kilimo na inapita kwa pembeni mbuga ya Kibasira kabla ya kuingia Mlimba na hatimaye Makambako.

Baada ya kupita maeneo ya Nyanda Juu za Kusini njia ya reli inaingia katika tambarare ya Usangu, na hapa hali ya hewa ni joto kidogo.
Kabla ya kufika Makambako, Hifadhi ya Milima ya Udzungwa inapanda hadi kufikia mita 2,137 kwa upande wa kaskazini na milima ya Kipengere upande wa Kusini.

Makambako ndiyo makutano ya reli na ile barabara kuu ya kwenda Zambia, na nyingine ikielekea Njombe na Songea. Baada ya Milima ya Kipengere, milima ya Uporoto inaonekana huku Bonde la Usangu likionekana upande wa kulia.

Kutokea Chimala reli inaambaa hadi Mbeya kwa upande wa kusini. Kutokea Mbeya reli inaendelea kusini-magharibi hadi Tunduma inapovuka mpaka na kuingia Zambia.

Source : Gazeti la RAI
 
Mmesahau habari za contolnumber JPM atabaki kuwa Rais Bora kwangu Leo hii nalipia baadhi ya huduma nikiwa na imani kuwa nachangia taifa langu sio kile kipindi cha vijesenti watu wanabeba Hela kwenye sandarus na Hakuna maendeleo yoyote taliyofanywa twiga kukwea pipa Mzee nitakukumbuka Sana
 
Mradi wa reli unafaida kubwa,kwanza Barbara zetu hazitaharibika Tena kwasababu mizigo mikubwa itakuwa ikibebwa na treni na ivyo kupunguza gharama za ukarabati WA marakwamara WA Barbara pia mizigo kusafirishwa Kwa muda mfupi tofauti na njia ya malori
Kupunguza ajari kwani malori yamekua Kero barabarani.
Kupunguza gharama za kusafiri na muda WATANZANIA watasafirisha bidhaa zao na biashara zingine Kwa gharama nafuu na speed kubwa Leo hii Mwanza to Dar ni masaa karibu 16
 
Walikaa kama kobe kipindi wanapitishwa bila kura kuhesabiwa pumbavu sana hawa
 
Back
Top Bottom