Mbunge adai Wilaya ya Ushetu haina jengo la Kituo cha Polisi wala nyumba za Askari

Mbunge adai Wilaya ya Ushetu haina jengo la Kituo cha Polisi wala nyumba za Askari

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760


WILAYA YA USHETU HAINA JENGO LA KITUO CHA POLISI WALA NYUMBA ZA ASKARI
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mkoani Shinyanga, Emmanuel Cherehani amesema Wilaya yake haina jengo lolote la Kituo cha Polisi wala hakuna nyumba za Askari ambapo wanatumia mfumo wa kupanga kwenye majengo ya watu na taasisi nyingine.

Akifafanua hali hiyo, Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amesema “Ushetu ni Wilaya mpya ilimegwa kutoka Kahama na hiyo changamoto ipo, wanahitaji Kituo cha Polisi cha uhakika kutokana na shughuli za kiuchumi zinazoendelea, hivyo pale tutakapopata fedha kituo hicho kitajengwa.”

BASHE AWASILISHA BAJETI YA KILIMO
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameliomba Bunge kuidhinisha zaidi ya shilingi Bilioni 970 kwa ajili ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Akisoma bajeti ya wizara hiyo Bungeni, Dodoma Waziri Bashe amesema fedha hizo ni sawa na ongezeko la asilimia 29 zaidi ya bajeti ya mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Waziri Bashe amesema, fedha hizo zitapelekwa kwenye maendeleo ya sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali kama uzalishaji wa mbegu bora za kilimo na kuendelea na mpango wa Ujenzi wa Kesho Bora (BBT).

WIZARA YA KILIMO IMEKUSANYA 0.5% KATI YA TSH. BILIONI 126
Mwaka 2022/2023, Wizara ya Kilimo ilikadiria kukusanya mapato ya Tsh. 126,100,000,000 kupitia Fungu 05, kutokana na vyanzo mbalimbali, lakini hadi Aprili 2023, Wizara imekusanya Tsh. 679,574,980.00 sawa na asilimia 0.5 ya makadirio.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema ukusanyaji huo mdogo umechangiwa na kutokuwepo kwa Ofisi za umwagiliaji za Wilaya, kutokusajili skimu za umwagiliaji na wakulima, uelewa mdogo wa wakulima kuhusu umuhimu wa ada ya huduma za umwagiliaji.

Pia ukosefu wa mfumo wa kielektroniki wa makusanyo na ukosefu wa wahandisi wa umwagiliaji wa wilaya ambao ndio wenye jukumu la msingi la ukusanyaji wa maduhuli hayo
 
Back
Top Bottom