Mbunge Agnes Marwa ashiriki maadhimisho ya siku ya wanawake musoma vijijini

Mbunge Agnes Marwa ashiriki maadhimisho ya siku ya wanawake musoma vijijini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Agnes Marwa amefanya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa kutembelea Kituo cha Afya Mugango na kutoa Misaada mbalimbali kwa akina mama wenye uhitaji.

Akiwa ameambatana na kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Musoma Vijijini chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Jane Chongo, Madiwani wa Viti Maalum na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali.

Maadhimisho hayo yametanguliwa na Semina ya ukatili wa kijinsia kwa akina Mama iliyotolewa na Jeshi la Polisi Dawati la jinsia na kufuatiwa na utoaji wa Misaada mbalimbali kwa wahitaji.

Pia Mbunge amepata nafasi ya kufanya ziara katika Kituo cha Afya cha Mugango, na kutoa Misaada mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa Kituoni hapo na pia kuzungumza na uongozi wa Kituo hicho na kusikiliza changamoto zao ili kwenda kuzitafutia Ufumbuzi.

Huku akiwahimiza watendaji wa Kituo kufanya kazi kwa Weledi, bidii na Upendo ili kuendelea kupunguza Vifo vya Mama na mtoto, ikiwa ni Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Katika maadhimisho hayo pia Mbunge ametoa Mashine ya Printa, Sare za Chama kwa Jumuiya ya UWT Wilaya ya Musoma vijijini na kuwataka kufanya kazi kwa Umoja, Bidii na Ushirikiano ili Kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Mkoani Mara.

Hayo yamefanyika ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani tarehe 8 Machi, 2023.

WhatsApp Image 2023-03-03 at 07.42.15.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-03 at 07.42.16.jpeg
WhatsApp Image 2023-03-03 at 07.42.15(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-03-03 at 07.42.16(1).jpeg
 
Back
Top Bottom