Mbunge Agnes Marwa atoa sadaka maalum kuunga mkono maandalizi ya mwezi mtukufu wa Ramadhani

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Agnes Marwa, leo tarehe 16 Februari, 2026 ametoa sadaka maalum kwa viongozi wa dini ya Kiislamu katika Misikiti tofauti ya Musoma Mjini ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono maandalizi ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Sadaka hiyo imelenga kuwasaidia viongozi wa dini pamoja na waumini katika kujiandaa na mwezi huo muhimu wa ibada, unaoheshimiwa na Waislamu duniani kote. Baadhi ya vitu vilivyotolewa ni pamoja na buswati, tende, kanzu, balaghashee pamoja na fedha taslimu, ambavyo vimekabidhiwa kwa viongozi kutoka misikiti mbalimbali ya Musoma Mjini.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Agnes Marwa alisema kuwa sadaka hiyo ni ishara ya mshikamano, upendo na heshima kwa viongozi wa dini, pamoja na kuthamini mchango wao katika kujenga maadili mema na amani ndani ya jamii.

“Nimeona ni muhimu kushiriki na ndugu zetu wa Kiislamu katika maandalizi ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Huu ni mwezi wa ibada, subira, na kusaidiana, hivyo ni wajibu wetu kama viongozi kuendelea kuwa karibu na jamii na kuunga mkono juhudi zao,” alisema Agnes Marwa.

Kwa upande wao, viongozi wa dini walipokea sadaka hiyo kwa shukrani kubwa, wakieleza kuwa msaada huo utasaidia katika maandalizi ya mwezi wa Ramadhani na kuimarisha zaidi mshikamano kati ya viongozi na jamii.

Hatua hiyo imepokelewa vyema na wananchi na waumini wa Dini ya kiislamu, wakieleza kuwa inaonyesha mfano wa uongozi unaojali na kuthamini imani, umoja na ustawi wa jamii ya Kitanzania

dd3a7c8e1d19454bb0a474fb99264417.jpg
8ad2d4eb75164de5a7f544a356336502.jpg
IMG-20260216-WA0107.jpg
7ecd3b5705914e0c959fb0ebc6d128d6.jpg
 
View attachment 3545039View attachment 3545040View attachment 3545041View attachment 3545042
kutoa ni moyo na wala sio utajiri,

well done MH.AGNES MARWA:KasugaYeah:
 
Back
Top Bottom