Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
KUNTI MAJALA AHOJI KWANINI TANGA CEMENT ILAZIMISHWE KUUZWA TWIGA CEMENT
Mhe. Kunti Majala, Mbunge wa Viti Maalum tarehe 04 Mei, 2023 alipata nafasi ya kuchangia suala la Tanga Cement na Twiga Cement wakati wa kuwasilishw akwa hoja ya bajeti ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara iliyosomwa na Waziri mwenye dhamana Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji
"Mfano mimi Kunti nikaona nimefilisika katika biashara yangu na sioni dalili huko mbele ya kuendelea nayo, nitatangaza ili nipate watu wengine mbadala waje wanunue, lakini ni kwanini sasa tunalazimisha Twiga Cement ndio iinunue Tanga Cement?" - Mhe. Kunti Majala, Mbunge Viti Maalum
"Mimi najiuliza tu kama mwekezaji wa Tanga Cement amefilisika na anaona hawezi kuendelea na biashara kwanini achague mtu wa kumuuzia hiyo biashara yake?. Nauliza tena hivi ni yeye (Tanga Cement) anachagua mtu wa kumnunua au Serikali ndio itamchagua mtu wa kumnunua" - Mhe. Kunti Majala, Mbunge wa Viti Maalum.