Mbunge ahoji ukimya wa Serikali kuhusu fidia ya waliopisha Reli ya SGR Tabora

Mbunge ahoji ukimya wa Serikali kuhusu fidia ya waliopisha Reli ya SGR Tabora

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Siku chache baada ya Mdau wa JamiiForums.com kuripoti juu ya malalamiko ya Wananchi wa Tambukareli, Kata ya Nsololo, Wilaya ya Uyui wanaodai malipo ya kupisha Mradi wa Reli ya Kisasa ya SGR kuchelewa kwa zaidi ya Mwaka mmoja na nusu, Mbunge wa Igagula, Venant Daud Protas amehoji juu ya hatma ya malipo ya Wananchi hao Bungeni, Mei 30, 2024.

Mbunge huyo ameelekeza swali hilo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa lakini Spika Tulia Ackson akasema hilo swali linapaswa kuelekezwa kwa Wizara husika.

Mdau alidai licha ya kufanyiwa tathimini tangu Machi 2023, hawajapokea malipo hadi sasa Mei 2024 na hawajui hatima ya malipo yao.

Ambapo, Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Zacharia Mwansasu alipoulizwa na JamiiForums alisema “Wananchi wanaolalamika wanatakiwa kufika ofisini kwa DC, namba yangu wanayo na nimeshazungumza nao mara kadhaa hadi katika mikutano ya hadhara nikiwa na TRC.”

Pia soma -

- Tabora – Uyui: Wananchi waliotakiwa kupisha Mradi wa SGR waomba Serikali isaidie walipwe fidia zao

- Mkuu wa Wilaya: Wananchi wa Uyui wanaodai malipo ya kupisha Mradi wa SGR wafike ofisini
 
Back
Top Bottom