BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mbunge wa Ilemela (CCM), Dk Angelina Mabula ameitaka Serikali kujenga uzio katika Shule ya Msingi Kitangili iliyopo mkoani Mwanza ili kuokoa maisha ya watoto wanaochezea kondomu katika uwanja wa mpira.
Akiuliza swali la nyongeza bungeni leo Jumanne Aprili 23, 2024, Dk Mabula amesema eneo hilo lenye shule mbili nyakati za usiku limekuwa likitumiwa na dada poa na lipo katika uwanja wa CCM wa Kirumba.
“Ni lini Serikali itaweka uzio ili kuokoa maisha ya watoto ambao wanachezea mipira (kondomu), “amehoji Dk Mabula.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala Bora na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Zainab Katimba amemkumbusha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilemela kwenda katika shule hiyo na kufanya tathmini.
“Kama alivyozungumza mheshimiwa mbunge kuna kila sababu ya halmashauri kupitia mapato yake ya ndani kutenga fedha ili kunusuru na kutengeneza mazingira bora ya wanafunzi hao,” amesema.