Mbunge wa jimbo la Same Mashariki Anne Kilango Malecela ameandika na kusambaza kwa wananchi kitabu chenye kurasa 139 Kinachoeleza miradi ambayo imetekelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika jimbo hilo.
Akizungumza wakati wa uwasilishaji wa utekelezaji wa ilani ya CCM ya Mwaka 2020-25 katika jimbo hilo, Kilango amesema katika kipindi cha miaka minne ya Rais Samia amefanya mambo mengi ikiwemo barabara ya Ndungu-Mkomazi-Same.