Mbunge alipwe mshahara na Wananchi wa Jimbo lake

Mbunge alipwe mshahara na Wananchi wa Jimbo lake

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Kumezuka mjadala kuhusu mishahara ya Wabunge na Posho zake, ambapo wabunge wanalalamika kuwa wanalipwa pesa kidogo na huku wananchi wakilalamika kuwa kodi zao zinachezewa bure ili kuwalipa wabunge mishahara mikubwa na posho zisizokuwa na kichwa wala mkia.

Sasa ili kukata mzizi wa fitina, ni wakati sasa wa wananchi wa jimbo husika kuamua mbunge wao na diwani wao walipwe mshahara na posho kiasi gani.

Bungeni pabakie kuwa mahali pa kujadili mambo mengine muhimu ya kitaifa, na kamwe pasiwe mahali pa kwenda kuvuna mishahara na posho.
 
Halafu tutanunuaje wajumbe?
Mtakuwa mmetukaba tunaojiita wazalendo.
CCM HOYE
 
Yule mbunge ni zwazwa hii ndo athari ya watu ambao hawakuchaguliwa na wananchi kuwa viongozi
 
Mshahara wa wabunge ukaweke PE Kwanza. Mjadala mwingine uanzie hapo
 
Back
Top Bottom