Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Vijana Taifa, Mhe. Amina Ali Mzee akichangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Ujenzi ametoa wito kwa Taasisi za Serikali kulipa madeni wanayodaiwa na Mashirika ya TBA na TEMESA ili kupunguza changamoto za ukosefu wa fedha kwa Mashirika hayo.
"Nampongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi katika sekta ya ujenzi. Tunaona mtandao mkubwa wa Barabara ndani ya Tanzania unaendelea kuenea" - Mhe. Amina Ali Mzee, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa
"Naipongeza Wizara ya Ujenzi kwa kuendelea kuwapa Wakandarasi vijana na wanawake wanaomaliza Chuoni kuwajengea uwezo wa miaka mitatu ili waweze kujiajiri katika kazi mbalimbali ambazo ni za barabara zinazoendelea nchini" - Mhe. Amina Ali Mzee, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa
"Naomba Serikali ione namna ya kuwawezesha Shirika la TBA ambalo linajitahidi kujenga nyumba ambazo wananchi na watumishi wanaishi ndani ya Dodoma na maeneo mengine nchini. Kamati ya Bunge imeshauri TBA ipewe Shilingi Bilioni 50 ili waweze kujiendesha kibiashara na kuzalisha faida" - Mhe. Amina Ali Mzee, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa
"Taasisi nyingi za Serikali zinadaiwa na TBA ambazo zinazidi kuikwamisha TBA kujiendesha yenyewe kwa faida na biashara. Wapo baadhi ya Wabunge na Wananchi wanaodaiwa na TBA. Nitoe wito kwa wananchi na taasisi za Serikali ziweze kulipa madeni ambayo wanadaiwa na TBA"
"Taasisi nyingi za Serikali na Wizara wanapeleka magari yao ya Halmashauri ndani ya TEMESA lakini wakishapeleka wanaigeuza TEMESA kama shamba la Bibi, wakishapewa huduma wanaondoka na magari yao lakini TEMESA hawailipi"
"Natoa wito Taasisi za Serikali kuilipa TEMESA madeni yao, TEMESA inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa Vifaa kama Vipuli. Serikali ione haja ya kuwapatia mtaji TEMESA ili waweze kununua Spea wenyewe bila kutegemea kutoka kwa wafanyabiashara
"Taarifa ya Kamati ya Bunge (Miundombinu) imeeleza wananchi wengi wanadai fidia, naomba Serikali tuchukue hatua za haraka kuhakikisha wananchi wetu wanalipwa fidia waliopisha ujenzi wa barabara" - Mhe. Amina Ali Mzee, Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa.