Mbunge analipwa mshahara wa 3.8M kwa mwezi, anapata posho 8M kila mwezi, jumla 11.8M. Akiwa kwenye kikao analipwa posho ya kikao 240K

Mbunge analipwa mshahara wa 3.8M kwa mwezi, anapata posho 8M kila mwezi, jumla 11.8M. Akiwa kwenye kikao analipwa posho ya kikao 240K

SOPINTO

Senior Member
Joined
Oct 19, 2020
Posts
155
Reaction score
387
Mbunge analipwa mshahara wa 3.8M kwa mwezi, anapata posho 8M kila mwezi, jumla 11.8M. Akiwa kwenye kikao analipwa posho ya kikao 240K kwa siku na posho ya kujikimu 120K, jumla 360K. Bunge la bajeti litakaa kwa miezi mitatu, akihudhuria vikao vyote atapata 32M, wastani wa 10M kwa mwezi. Kwahiyo hii miezi mitatu ya bunge la bajeti Mbunge ana uhakika wa kukunja 22M kila mwezi.

Sambamba na hayo anapewa mkopo wa 90M kwa ajili ya gari na bima ya afya daraja la kwanza inayomruhusu kutibiwa yeye na familia yake ndani na nje ya nchi. Anapewa lita 1,000 za mafuta kila mwezi. Vyote hivyo havikatwi kodi. Mtumishi mwenye mshahara wa laki mbili, anakatwa kodi, anakatwa mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF/PSSSF), anakatwa bima ya afya, LAKINI Mbunge mwenye karibu 12M kwa mwezi, na marupurupu kibao hachangii chochote kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, hachangii kodi, wala hachangii bima ya afya.

Baada ya miaka mitano, Mbunge huyohuyo anapewa kiinua mgongo cha 240M, ambacho hakuwahi kukatwa kuchangia hata mwezi mmoja. Je pesa hizi za kiinua mgongo anazolipwa zinatoka wapi kama alikua hakatwi? Jibu ni.kwamba zinatoka kwa watanzania maskini including wale wanaolipwa laki mbili kwa mwezi.Halafu Mbunge mmoja bila aibu anademka eti watanzania walipe tena kodi kwa kutumia simu zao. Yeye anaiita kodi ya uzalendo na ameshauri ilipwe kila siku. Yani kila ukiamka unakatwa kiasi fulani cha pesa kwenye simu yako kama kodi ya uzalendo.

Wabunge walipaswa kuonesha mfano wa uzalendo. Wakatwe kodi kwenye mishahara yao na posho zao zote. Mbunge akiangalia salary slip yake aone Gross salary ni 11.8M lakini Net saalary ni 7M. Akatwe Bima ya afya, akatwe pensheni pia. Hapo atakua na adabu na ataongea lugha moja na wananchi, maana atakua anafeel kile wananchi wake wanafeel.

Na akipoteza ubunge akiwa na miaka 30 asubirie hadi afikishe miaka 60 ndipo apate mafao yake. Wale wanaopoteza ubunge wakiwa na mika zaidi ya 60 ndio wapewe mafao yao kwa wakati. Na wapewe kwa kadri walivyochangia kwenye mifuko ya hifadhi za jamii. Kama alikua anakatwa 500K kwa mwezi kwa ajili ya pensheni means baada ya miaka mitano atakua amechangia 30M. Hiyo ndio haki yake, lakini asipewe hadi afikishe miaka 60.

Hapa ndio tutaona kweli ni wazalendo. Sio wanatunga sheria za kiiimla kukandamiza wanyonge, halafu wao wanajiondoa kwenye sheria hizo. Wanaishi kwenye dunia yao halafu wakishavimbiwa nyama choma na Dompo wine, wanabweka kuhusu uzalendo. Uzalendo gani wakati umezuia fao la kujitoa kwa vijana maskini, while wewe unavuta mshiko kila baada ya miaka mitano?

Unatunga sheria kuwa kijana maskini aliyetoka chuo akapata ka mkataba ka miaka miwili, akimaliza mkataba wake eti asilipwe mafao yake hadi afikishe miaka 60. Lakini wewe ukipoteza ubunge na miaka 35 unataka uvute mafao yako fasta. Hutaki kusubiri ufikishe miaka 60. Huu ndio uzalendo mnaohubiri?

Halafu hawa watanzania unaotaka walipe kodi ya uzalendo kupitia simu zao ni wapi? Hawahawa maskini au kuna wengine? Tanzania ina watumiaji wa simu za mkononi milioni 40. Kati yao watanzania milioni 8 matumizi yao kwenye simu hayafiki TZS 1,000/= kwa mwezi. Yani kuna watanzania milioni 8 ambao ndani ya mwezi mzima hawawezi kutumia "buku" kwenye simu. Hawa ndio wanataka kukamuliwa kodi ya uzalendo na watu wanaolipwa 12M kwa mwezi.
 
Ni wizi mkubwa sana mwanzo mwisho.
Nimesikiliza hotuba ya mama Samia. Ni bla bla kama bla bla nyingine tu za wakati wa kampeni. Kufanya mabadiliko kwenye hii system tuliyonayo ni kama kujidanganya. Hebu ona mbunge anavyomega pato la nchi. Na bado kuna maeneo mengine mengi sana amabyo fedha zinamegwa sana.

Rais atakayeleta mabadiliko ni rais atakayekubali kufumua system na kuondoa mianya kama hii. Taifa letu linaingiza pato zuri tu ila vipaumbele imekuwa mifuko ya wanasiasa. NB: Na hapo hujaweka usafiri wa daraja la pili kwenye ndege.
 
Mkuu kwa maoni yangu ili kuinusuru nchi yetu na hawa wahuni na mafisadi ni lazima tupate Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi vinginevyo ni vilio vya kusaga meno vitaendelea nchi nzima na kwa miaka mingi ijayo.
Nimesikiliza hotuba ya mama Samia. Ni bla bla kama bla bla nyingine tu za wakati wa kampeni. Kufanya mabadiliko kwenye hii system tuliyonayo ni kama kujidanganya. Hebu ona mbunge anavyomega pato la nchi. Na bado kuna maeneo mengine mengi sana amabyo fedha zinamegwa sana. Rais atakayeleta mabadiliko ni rais atakayekubali kufumua system na kuondoa mianya kama hii. Taifa letu linaingiza pato zuri tu ila vipaumbele imekuwa mifuko ya wanasiasa. NB: Na hapo hujaweka usafiri wa daraja la pili kwenye ndege.
 
Back
Top Bottom