Mbunge analipwa mshahara wa 3.8M kwa mwezi, anapata posho 8M kila mwezi, jumla 11.8M. Akiwa kwenye kikao analipwa posho ya kikao 240K

Hivi na wale waliopo kwenye kamati maalum mathalani utaskia kamati ya madini, viwanda, kilimo, maji n.k.
Wale wapuuzi kila ziara wanayofanya kuna kiasi cha pesa wanatia matakoni.
 
Ndugai alimchapa mpinzani wake fimbo mpaka akapoteza fahamu lakini still akapewa kazi ya kuongoza mhimili inayotakiwa kutunga sheria yenye kuleta usawa!!! inafikirisha sana kwakweli.
Hakuwajibishwa na chama kuhusu nidhamu wala hakuchukuliwa hatua za kisheria na vyombo vyetu.

Huyu mtu ndiye anatakiwa kutusemea matatizo yetu sisi wananchi; hatuko sawa kichwani.
Bunge linahitaji kuwajibishwa na wananchi.
 
Siku waTanzania wakipata kujua rangi halisi za wanasiasa wao ndio litakapoanza vugu vugu la kweli mageuzi ya kimfumo hapa nchini........na hilo vugu vugu halitangoja hata tamko la mwanasiasa yeyote kwani automatically kila mwananchi atajikuta kuwa ni muhanga kwa namna moja au nyingine wa matendo maovu ya wanasiasa.....
 
Hawa fisi dawa yao ni kuandamana tu kila mtu na vitoto vya nguruwe na kwenda kuwatupia pale Mjengoni! Yaani mpaka Mama leo kaamua awatolee uvivu kwa kuwataka waikosoe serikali kadiri iwezekanavyo, baada ya kugundua wengi wao hutumia muda mwingi kumsifia magufuli na utawala wake wa kusadikika.
 
Usisahau hata ndugu zetu kina Lema, Mbowe, Sugu, Msigwa, Lissu nk walikuwepo bungeni miaka takribani 10 wakienjoy package hiyo hiyo iliyonona
HIZI PACKAGE ZA NAMNA HII NDIO ZINAWASHAWISHI WATAALAM WAACHE TAALUMA ZAO NA KUKIMBILIA KWENYE SIASA, NA HILO HALINA TIJA KWA NCHI. MISHARAHA YOTE NCHINI IWE NA UWIANO ILI WANANCHI KILA MMOJA ABAKI KWENYE PROFESSION YAKE BADALA YA SASA AMBAPO MADAKTARI BADALA YA KUTIBU WAGONJWA WANAKWENDA KUPIGA MAKOFI BUNGENI AMBAKO WANAVUTIWA NA MISHAHARA!!
 
Mkuu kwa maoni yangu ili kuinusuru nchi yetu na hawa wahuni na mafisadi ni lazima tupate Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi vinginevyo ni vilio vya kusaga meno vitaendelea nchi nzima na kwa miaka mingi ijayo.
Hahahaha
 
Tunaongelea umma na sio private company. Au mbunge anafanya kazi za kampuni binafsi siku hizi?
 
Zungu na wenzake wanaovimba matumbo bungeni wajue hayo
 
Kwanini hujamtambua mwandishi wa hii?? Kama wewe sio Malisa Gj basi unachofanya kukopi andiko la mwenzio na kulibandika bila kumtaja yeye anaita UGIGISI.

Shule mlisomea ujinga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…