Mbunge analipwa mshahara wa 3.8M kwa mwezi, anapata posho 8M kila mwezi, jumla 11.8M. Akiwa kwenye kikao analipwa posho ya kikao 240K

Hiki ni Chanzo kingine cha serikali kukusanya kodi, kisipuuzwe kwani kila chanzo na hasa kinachoweza kulipwa na mlipakodi ni muhimu kufikiwa bila kujali nafasi zao ktk jamii.

Ujumbe, wabunge lipeni kodi mchangie gharama za huduma kama ulinzi, usalama, afya na miradi ya maendeleo.
 
Na Rais nae alipe kodi! Haiwezekani na yeye anatuletea maneno matamu ya kulipa kodi kwa hiyari, huku yeye mwenyewe pamoja na hao Wabunge wakiishi maisha ya peponi, haafu hawalipi kodi!

Kila mtu ndani ya nchi alipe kodi! Kuanzia kwa Rais mwenyewe, Wabunge, Mawaziri, wafanyakazi, wakulima, wafanyabiashara, bodaboda, mamantilie, wamachinga, nk. Wote tulipe kodi.
 
Pamoja na hayo mkuu wabunge huchangia pesa nyingi kwenye majimbo yao kuanzia misiba,wenye shida mbalimbali sasa unadhani hiyo michango mikubwa bila hiyo pesa wataiweza, labda utakuwa huishi kwenye majimbo yaliyo nje ya Darisalama,kama ungekuwa huku vijijini ungeona jinsi wabunge wanavyotoa michango yao kwenye shughuli nyingi za wapiga kura wao, naamini pia kama una uwezo watu wanaokupiga mizinga kila siku ni wengi ,huyu atakuomba hiki na mwingine kile. Watu wengi wanaolaumu ndio hao hao kila siku wamekuwa ombaomba kwa watu wenye vipato wakiwemo wabunge.
 
Nasikia kuwa wabunge wako kwenye kundi la wasiokatwa kodi. Kama ni kweli ni kwanini?

Nchi yetu bado ni changa, kama kweli tuko serious tunataka kuijenga nchi yetu wabunge lazima waonyeshe uzalendo kwa kukatwa kodi ya mapato.
Hiyo ni hoja nzuri. Kwa nini wao was iwe mstari wa mbele kuwa mfano... Badala ya kuhubiri Uzalendo bila vitendo. Hakuna justification yeyote kwa nini wasikatwe kodi hasa kwenye mshahara wao.
 
Ubunge mtamu jamani! Yani imagine ndani ya mwaka tu unaweza kumeki ukajenga mjengo wako wa maana na life likabadilika mazima😂😂😂!

Ukikaa miaka mitano kisha ukaongeza mingine mitano basi dunia nzima ni yako hapo unaweza hata kumtukana mtanzania hohehahe kwa kumlazimishia kodi ya simu!
 
Hakuna mahali duniani ambapo posho inazidi mshahara... Only in TZ.
 
Itakuwa vipi wakiongezwa mishahara halafu ndio wakatwe kodi. Tutarudi pale pale
 
Hapo ukiwagusa mkuu unaambiwa wanaombwa hela mno na wananchi mtaani ndio maana wanatunishiwa mfuko..
 
Mimi ndo hapo sielewi kabisa logic inayotumika kuwasamehe wanasiasa(Wabunge n.k) wasilipe Kodi ya mapato(Income Tax).Ikiwa hata boda boda,na wenye mishahara kidogo kabisa Serikalini na kwenye private sectors wote Hawa walala hoi wanalipa Hiyo Kodi,Hawa wabunge wanaolipwa she 12,000,000 kwa mwezi,Ni kwa nini wasilipe Kodi?

HIZI NDIZO BAADHI YA DHAMBI KUBWA WANAZOTENDA WANADAMU LAKINI HAWAJUI KWAMBA NI DHAMBI.Msipotubu dhambi hii na kumrudia Mungu kwa kulipa hii Kodi,mjue siku ya MWISHO mnayo hoja ya kujibu mbele ya MUNGU.

"Walafi wote hawataingia katika ufalme wa Mungu.Maana huu Ni sawa TU na ulafi,
 
Nlichogundua hatutakaa tutoke hapa tulipo ikiwa tutakosa njia ya kuwaadabisha wanasiasa, kadiri wanavyofanya maamuzi ya hovyo na sisi kushangilia ndivyo wanavyotuona mazoba, i wish lifanyike jambo siku moja ili hawa kundi la mchwa na Viwavi Jeshi watuheshimu, kila kitu kipo juu na wakamuliwa ni sisi walala hoi.

Ukiangalia mafita ya kula bei juu, petroli bei juu, bando ndio usiseme lkn kuna kakundi la Wanyonyaji wanakula na familia zao na kusaza, we need Action now sio kupiga domo, hakika tumeliwa
 
Na Rais nae alipe kodi! Haiwezekani na yeye anatuletea maneno matamu ya kulipa kodi kwa hiyari, huku yeye mwenyewe pamoja na hao Wabunge wakiishi maisha ya peponi, haafu hawalipi kodi!..
Tutanue wigo wa kukusanya kodi kwa wabunge pia kutozwa kodi kwenye mapato yao, huo ndio uzalendo kwa taifa. Uzalendo sio kuvaa tai, bags, skafu au shati lenye rangi za bendera.
 
Ninapata uchungu kwa kuona watu tunaowapigia kura waende wakatutetee bungeni wanakwenda kuungana na serikali kupitisha sheria zinazowakandamiza au kuondoa haki za jamii huku wao wakijiwekea kinga ya kutobanwa na sheria.

Kodi tulipe wote kusiwepo na kundi la watu wanasamehewa kwa vyeo vyao , vinginevyo tunathibitisha kuwa mwenye nacho ataongezewa na asiyekuwa nacho atanyang'anywa hata kile kidogo alicho nacho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…