Kijogoodi
JF-Expert Member
- Mar 29, 2021
- 1,362
- 2,373
Kutokana na uzalishaji mkubwa wa mahindi uliofanyika mwaka huu na kupelekea bei ya mahindi kushuka sana, mbunge wa Namtumbo Vitar Kawawa ameiomba serikali itoe fedha inazopewa kama msaada wa kupambana na Corona kwenda kupambana na upungufu wa bei za wakulima ambao ni wanyonge na ikizingatiwa bei ya mbolea imepanda sana badala ya kuzikumbatia hizo hela kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa kusadikika.