#COVID19 Mbunge aomba pesa za COVID-19 zitumike kununua mahindi ya wakulima

Kutokana na uzalishaji mkubwa wa mahindi uliofanyika mwaka huu na kupelekea bei ya mahindi kushuka sana, mbunge wa Namtumbo Vitar Kawawa ameiomba serikali itoe fedha inazopewa kama msaada wa kupambana na Corona kwenda kupambana na upungufu wa bei za wakulima ambao ni wanyonge na ikizingatiwa bei ya mbolea imepanda sana badala ya kuzikumbatia hizo hela kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa kusadikika.

Bora tutapata hela tayari
 
Wazo zuri sana ila atachukiwa na kuzushiwa zengwe na wenzie. Tetea wananchi hata kama watakufukuza utakuwa umetimiza wajibu wa kuwawakilisha wananchi wasio na kura ya veto hata kwenye uchaguzi veto yao inamwagiwa tindi-kali
Safi
 
Kwanza yeye Alisha chanja?kwa sababu adhabu iliyotolewa kwa gwajima wabunge wote waliunga mkono,kana kwamba wote wanaku baliana na kuchanja lasivyo inabidi wabunge wote wachanjwe kwa lazima.
 
Kutokana na uzalishaji mkubwa wa mahindi uliofanyika mwaka huu na kupelekea bei ya mahindi kushuka sana, mbunge wa Namtumbo Vitar Kawawa ameiomba serikali itoe fedha inazopewa kama msaada wa kupambana na Corona kwenda kupambana na upungufu wa bei za wakulima ambao ni wanyonge na ikizingatiwa bei ya mbolea imepanda sana badala ya kuzikumbatia hizo hela kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa kusadikika.

Halafu siku waliotoa hiyo misaada yakianza kuhoji pesa yao mnawaita mabeberu na wanawapiga vita
 
Back
Top Bottom