Mbunge ashauri kuwepo Sera ya Watanzania wenye nyumba za bati kuvuna maji ya mvua

Mbunge ashauri kuwepo Sera ya Watanzania wenye nyumba za bati kuvuna maji ya mvua

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini, Dkt. Alfred Kimea ameshauri Wizara ya Maji kutengeneza Sera itakayowafanya Watanzania wawe na tabia ya kuvuna maji ya mvua

Akichangia katika Bajeti ya Wizara ya Maji Bungeni amesema, "Kila Mtanzania mwenye nyumba ya bati tayari ana chanzo cha Maji, kinachobaki ni storage (hifadhi) tu"

Ameeleza, endapo Watanzania wenye nyumba za bati watatambua tayari wana chanzo cha maji, tatizo hilo litapunguzwa kama sio kumalizika Nchini
 
Tatizo ni hela. Kuvuna maji sehemu zenye mvua ni faida kubwa, ambapo hayo maji unaweza kuyatumia kwa matumizi ya ziada mfano bustani, hivyo kupunguza bili.

Sijajua simtank ni sh ngapi? Ila nina uzoefu na tank la chini ya ardhi la kujenga kwa matofali ambapo kwa mbangaizaji mwenye kijumba cha cha bati-chumba kimoja na sebule hawezi kumudu kulijenga, labda kama alikuwa anawazungumzia matajiri wanaoishi kwenye mahekalu, hao ni vyema wavune maji.
 
Back
Top Bottom