Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini, Dkt. Alfred Kimea ameshauri Wizara ya Maji kutengeneza Sera itakayowafanya Watanzania wawe na tabia ya kuvuna maji ya mvua
Akichangia katika Bajeti ya Wizara ya Maji Bungeni amesema, "Kila Mtanzania mwenye nyumba ya bati tayari ana chanzo cha Maji, kinachobaki ni storage (hifadhi) tu"
Ameeleza, endapo Watanzania wenye nyumba za bati watatambua tayari wana chanzo cha maji, tatizo hilo litapunguzwa kama sio kumalizika Nchini