Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Nashoni ameyasema hayo Oktoba 24, 2021 wakati akizungumza katika semina ya kuangalia namna bora ya kuboresha huduma za afya iliyoandaliwa Taasisi ya Benjamin Mkapa na kuwahusisha wajumbe wa kamati mbili za Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na Utawala na Serikali za Mitaa.
Akichangia mjadala huo Bidyangunze amesema kwa mujibu wa mwezeshaji katika semina hiyo kuwa watoto 8,000 wanapata ujauzito karibu kila mwaka nchini.
“Nilikuwa natafakari katika eneo hilo la watoto wanapata mimba basi Serikali iweke mtaala ambao unawafundisha watoto kujua kalenda. Kwa sababu huwezi kuzuia hili jambo la watu wawili kukutana faragha kujamiana,” amesema.
Amesema kwa kuwa sio rahisi kulizuia hilo basi kuwepo na elimu itakayofundisha masuala ya uzazi ili kuwapa watoto ufahamu ni wakati gani mimba inaweza kuingia.
“Yes (ndio) wakijua hili la kalenda basi mimba zitapungua, lakini bila elimu unakutana naye leo kumbe ndio siku ya mimba. Kumbe angesubiri kidogo asingepata mimba. Ukweli unabakia pale pale,” amesema mbunge huyo.
Amesema hata Serikali ilipofikia mahali pakutambulisha suala la matumizi ya kondomu kuna watu walishangaa na kuhoji kuwa ni vipi Serikali inahamasisha kujamiana, lakini jambo hilo lilikuwa lina maana kwamba kondomu ikitumika itasaidia watu wasipate magonjwa,” amesema Bidyangunze.
Chanzo: Mwananchi