Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Mbunge wa Handeni Mjini Reuben Kwagilwa Reuben ameshauri viongozi kutumia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Kwaresma kukutana na makundi mbalimbali ya wadau katika kufuturisha kuweza kujadili maendeleo ya maeneo yao.
Akizungumza na viongozi dini,siasa na wananchi nyumbani kwake kwenye shughuli ya kufuturisha aliyoandaa amesema ni vizuri kujiwekea muda wa kupokea maoni ya wale wanaowaongoza.
Katibu wa CCM wilaya ya Handeni Mayasa Kimbau amepongeza hatua hiyo kwani ni wengi wenye uwezo ila hawakuweza kujaaliwa kukutanisha watu eneo moja na kubadilishana mawazo.
Diwani kata ya Kwenjugo Twaha Mgaya amesema kukutanishwa viongozi wa dini zote na wananchi pamoja na kubadilisha mawazo ni jambo jema na linatakiwa kuendelezwa siku zote kwani linaleta umoja.
Waumini wa dini ya Kiislam wapo kwenye mfungo wa Ramadhani huku Wakristo wakiwa kwenye Kwaresma.