PendoLyimo
JF-Expert Member
- Sep 30, 2014
- 969
- 1,055
Leo Mbunge wa Viti Maalum Vijana Mhe. Asia Halamga akiwa Mgeni Rasmi amefanya Uzinduzi wa Vijana Jogging Club Mkoa wa Kilimanjaro ambao una Kauli Mbiu "Amani Yetu, Maisha Yetu, Chukua Tahadhari Dhidi ya UVIKO-19"
Akizungumza na Vijana mbalimbali waliojitokeza kwa wingi kushiriki uzinduzi huo amewataka kuendelea kuchukua Tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona ili kuutokomeza nchini ikiwemo kufanya mazoezi, kula chakula bora (lishe bora) kuendelea kunawa Mikono kwa sabuni na maji tiririka, kuepuka misongamano isiyo yalazima na kujitahidi kuvaa barakoa.
"Tunafahamu chanjo ya UVIKO-19 ni hiari na Serikali imejiridhisha katika hilo,Serikali haiwezi kumuumiza mwananchi wake,kila mtu achukue tahadhari na kuongeza kufanya mazoezi na vijana wanaushawishi mkubwa kwa makundi mengine kushiriki"
Uzinduzi huo umeudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanjaro Mkoa na wilaya.