Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Jimbo la Busokelo, Mhe. Atupele Mwakibete, amechangia mchango wa shilingi Milioni 10 kw ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo la Busokelo.
"Hii ni kutokana na changamoto ambazo wanachama wanakutana nazo wanapohitaji huduma za Chama, ambapo walikuwa wanalazimika kusafiri umbali wa Kilomita 50 kufuata huduma hizo wilayani Rungwe" Mhe. Atupele Mwakibete
Aidha, Mwakibete amewataka wadau mbalimbali kuendelea kutoa michango katika shughuli za maendeleo ili kuhakikisha huduma kwa wanachama wa CCM katika jimbo la Busokelo zinakuwa rahisi na za haraka.