Pre GE2025 Mbunge atupele Mwakibete afanikisha kukusanya Milioni 27, harambee Kwaya ya KKKT usharika wa Kandete Mwakaleli

Pre GE2025 Mbunge atupele Mwakibete afanikisha kukusanya Milioni 27, harambee Kwaya ya KKKT usharika wa Kandete Mwakaleli

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Jimbo la Busokelo,Atupele Fredy Mwakibete ameongoza kukusanywa zaidi ya Shilingi Milioni 27 katika harambee ya Ununuzi wa gari aina ya Coastar ya Kwaya kuu ya Usharika huo.

Akizungumza kwa niaba ya Mgeni rasmi ambaye ni spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mwakibete amesema kuwa risala iliyosomwa na kukabidhiwa ataiwasilisha kwa Mheshimiwa Spika hivyo lolote atakalo ambiwa basi hatosita kutoa mrejesho.

Mbali na uwakilishi,Mheshimwa Mwakibete kama Mbunge na Mtumishi wa Busokelo ameshiriki sadaka hiyo ya Harambee kwa kutoa Shilingi Milioni 5.3(Milioni Tano na Laki Tatu) ili kuwaunga Mkono Kwaya Kuu KKKT Usharika wa Kandete Jimbo la Mwakaleli.

 
Huyu lazima ang'oke atake asitake LUSUBILO MWAKABIBI lazima achukue jimbo huyu mwakibete hafai hata kuwa mwenyekiti wa kitongoji yupo yupo kama zuzu tu. Nashangaa sana wananchi wa busokelo kumchamgua huyu bwana maana hana weled na ufanis wala sifa ya kuwa kiongozi
 
Back
Top Bottom