Mbunge au Diwani, akifa au kuhama chama, achaguliwe mwingine wa chama kile kile na kamati ya Wilaya au Mkoa. How does this sound?

Mbunge au Diwani, akifa au kuhama chama, achaguliwe mwingine wa chama kile kile na kamati ya Wilaya au Mkoa. How does this sound?

Hapana, wape wananchi haki ya kuchagua wanayemtaka, siyo kamati za watu. Quite undemocratic.

Ila kama watanzania kupitia sanduku la kura wamekubali utaratibu huo, it is well and fine.
Mbona Rais akifa makamu wake anamrithi bila uchaguzi?
 
Mbona Philip Mpango aliingia bila uchaguzi??..
Hata Philip Mpango kuingia bila uchaguzi haikutakiwa. Angalau angethibitishwa na bubge, lakini kwa upande mwingine kumthibitisha kiongozi wa pili katika ezecutive bungeni kuna matatizo yaje.

Rais na Makamu wake huchaguliwa pamoja. Hivyo akifa rais Makamu anachukua urais na kiti cha Makamu kinazibwa na mpaka sasa hatujapata mfumo mzuri wa kidemokrasia zaidi wa kukiziba cheo hicho.

Mfano kwa sasa akifariki Samia (siombei, natoa mfano tu), au kujiuzulu , Philip Mpango anakuwa rais bila kuchaguliwa hata kwa kura moja kuwa rais.

Ila kumteua Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais, mtu aliyekuwa mbunge na waziri, maana yake kashachaguliwa na watu kuingia bungeni ndiyo maana kaweza kuwa waziri, si sawa na kumteua mtu yeyote tu kuwa mbunge.
 
Marekani senator akijiuzulu, akiteuliwa kwa nafasi nyingine au akifariki Gavana wa jimbo anatea senator mwingine kujaza hiyo nafasi.
Really?? I didn't know this before. Na hao ndio matajiri na wanabana matumizi, sembuse sisi walalahoi..
 
..kwa nchi za dunia ya kwanza na at least dunia ya pili. Marudio ya chaguzi Kwa nchi za dunia ya tatu ni anasa mno mkuu..
si tunadai demokrasia? lakini kama unavyosema, lazima tuangalie uchumi wetu, mazingira yetu etc etc

(Out of context, but related.... ndiyo maana nasema katika fragile moments, Lisu ilibidi aangalie mazingira ya chama chake...CCM inakazana kukiua, wewe unaleta mfarakano eti ni demokrasia....nimemchukia kwa hilo ingawa alikuwa my very favorite politician)
 
Kumteua Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais, mtu aliyekuwa mbunge na waziri, maana yake kashachaguliwa na watu kuingia bungeni
Watu wa Jimbo lake tu na sio watanzania wa kila Jimbo..
 
Really?? I didn't know this before. Na hao ndio matajiri na wanabana matumizi, sembuse sisi walalahoi..
Gavana wa Illinois alifungwa miaka mingi tu gerezani alipotaka kuuza nafasi ya useneta ya Obama baada ya Obama kuchaguliwa Rais. FBI walimnasa katika njama za kuuza kiti cha useneta.
 
Mbona Rais akifa makamu wake anamrithi bila uchaguzi?
Economy class "riding"....inasaiia kuokoa pesa AU INGELIKUWA YULE ANAYEFUATIA KWA KURA NDIYO AKABE LOFU
 
Eti wadau, hii itasaidia kupunguza matumizi kwa hizi third world countries kama Tanzania?? How does this sound..

Mfano: Kafa Magufuli, akaingia Philip Mpango bila gharama za uchaguzi..

~ SIPENDI SIASA ~
Hatuchagui chama tunachagua Mtu, chama tofauti kinaweza kikawa na mtu mzuri kuliko chama cha yule alieondoka, Hii ni kwa nchi zenye uchaguzi, sio teuzi za Tanzania.
 
Hatuchagui chama tunachagua Mtu, chama tofauti kinaweza kikawa na mtu mzuri kuliko chama cha yule alieondoka, Hii ni kwa nchi zenye uchaguzi, sio teuzi za Tanzania.
Ulimchagua Philip Mpango kuwa makamu wa Rais??..
 
Eti wadau, hii itasaidia kupunguza matumizi kwa hizi third world countries kama Tanzania?? How does this sound..

Mfano: Kafa Magufuli, akaingia Philip Mpango bila gharama za uchaguzi..

~ SIPENDI SIASA ~
AU ALIYEFUATIA KWA KURA NDIYE AWE DIWANI, MBUNGE ETC ET HATA ILE YA URAIS INGELIKUWA HIVYO...ANAYEFUAT KWA KURA ZA WANANCHI
 
AU ALIYEFUATIA KWA KURA NDIYE AWE DIWANI, MBUNGE ETC ET HATA ILE YA URAIS INGELIKUWA HIVYO...ANAYEFUAT KWA KURA ZA WANANCHI
Hahahaaa, mkuu kwa hapa kuna michezo michafu ya "Cloak and dagger" inaweza kutumika kwa sababu hiyo aliyefuata kwa kura anajulikana lakini anayeweza kuchaguliwa na kamati hajulikani kwa maana contestants wanakuwa ni wengi (zaidi ya mmoja)..
 
Marekani senator akijiuzulu, akiteuliwa kwa nafasi nyingine au akifariki Gavana wa jimbo anateua senator mwingine kujaza hiyo nafasi.
Wanafanya hivyo, lakini huo si mchakato wa kidemokrasia.

Kitu kuwa kinafanyika Marekani haimaanishi kuwa ni cha kidemokrasia.

Ukifuatilia historia ya Obama alivyoacha kiti cha u Seneta Marekani kutoka jimbo la Illinois kwa sababu alikuwa rais mwaka 2008, Governor wa Illinois Rod R. Blagojevich alipata scandal kubwa sana ya kuuza kiti cha Obama.

Tayari hapo unaona mfumo wa kuteua replacement una mwanya mkubwa wa rushwa.

Starting in December 2008, a federal investigation and trial found Blagojevich guilty of public corruption after he attempted to sell the U.S. Senate seat vacated by Barack Obama upon his election to the presidency. Blagojevich was impeached, convicted, and removed from office in 2009 by the Illinois General Assembly.
 
Watu wa Jimbo lake tu na sio watanzania wa kila Jimbo..
Sawa, lakini hata Waziri Mkuu anachaguliwa na watu wa jimbo lake tu, lakini anakuwa Waziri Mkuu wa nchi nzima kwa msingi wa kuwa mbunge aliyechaguliwa na watu wa jimbo lake tu. At least in theory.

Point ni kwamba angalau amepitia kizingiti cha kuchaguliwa na wananchi kuwa mbunge.

Mtu wa kuteuliwa tu anaweza kuwa hajapitia kizingiti cha kuchagukiwa hata na mtu mmoja.
 
Back
Top Bottom