Mbunge Bahati Ndingo azungumzia mradi wa kilimo cha umwagiliaji katika bonde la Usangu

Mbunge Bahati Ndingo azungumzia mradi wa kilimo cha umwagiliaji katika bonde la Usangu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
"Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera, Nianze kwa kumshukuru Mheshimiwa Rais. Tumetajiwa mabilioni ambayo yanakwenda kuwekezwa. Mradi unakwenda kuwekeza zaidi ya Shilingi Bilioni 15, ni fedha nyingi. Tunaona dhamira ya dhati ya Mheshimiwa Rais kuhakikisha anafanya Wilaya ya Mbarali na bonde la Usangu kuwa sehemu yenye tija kwa uzalishaji wa chakula" - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge wa Jimbo la Mbarali

"Niwapongeze timu mnayomsaidia Mheshimiwa Rais ndani ya Mkoa wa Mbeya na ndani ya Wilaya ya Mbarali kwa kusimamia miradi vizuri, Hongereni sana. Sisi kama wananchi wa Mbarali tunaendelea kumshukuru Mheshimiwa Rais" - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge wa Jimbo la Mbarali

"Bado tuna miradi mingi ya umwagiliaji, tunatamani baada ya kukamilika miradi hii Wanambarali tuwe tunalima angalau mara mbili kwa mwaka na siyo kuzoea kulima wakati wa mvua tu, changamoto aliyoieleza Mheshimiwa Diwani, Mkuu wa Mkoa Tunaomba muichukue kwa uzito unaostahili kwasababu tunaambiwa kuna uwezekano tukapata mvua kubwa za El Nino" - Mhe. Bahati Ndingo, Mbunge wa Jimbo la Mbarali

WhatsApp Image 2023-10-28 at 09.29.18.jpeg
 
Back
Top Bottom