Kamakabuzi
JF-Expert Member
- Dec 3, 2007
- 2,903
- 1,360
Nimeongea na watu wengi wa Karagwe kuhusu kauli aliyosema bungeni mbunge wa Karagwe Blandes kuwa wananchi wa Karagwe wamemtuma kuwa wanakubali muswada wa tume ya katiba uliopo bungeni upite kama ulivyo, nao wamesema hawajawahi kumtuma chochote juu ya suala zima la katiba mpya.
Tangu mjadala wa mchakato wa katiba uanze wananchi wa Karagwe hawajawahi kuulizwa maoni yao na walikuwa wanamsuburi huyo mbunge awaeleze kama wao ni sehemu ya Tanzania au la kwa maana mwezi april muswada ulijadiliwa dsm, dodoma, na zanzibar kana kwamba tanzania nzima ni maeneo hayo matatu tu!
Wakati wanasubiri aje kujibu hoja hizo alishindwa kufanya hivyo kwa kusingizia eti hatakuwa na muda kwa sababu ya kuwa kwenye kamati ya bunge juu ya sakata la Jairo. Hivyo hakuzungumza na wananchi hao juu ya katiba.
Tangu hapo hajawahi kuja kuzumgumza na wananchi; wananchi wanasema hivyo kwa sababu pale alipokusudia kuja redio za wananchi (Radio Karagwe na Radio Fadeco) zilitumika kuwatangazia ujio wake na ratiba kamili, na tangia hapo hawajawahi tangaziwa kuwa mbunge atafanya ziara yoyote, hadi muswada ukapelekwa bungeni kusomwa kwa mara ya pili.
Kwa hiyo wananchi wa Karagwe hawajawahi kujadili muswada huo na mbunge wao, na wala hawajawahi kumtuma akubali muswada wa sasa.
Tunamtaka Blandes afute kauli yake haraka iwezekanavyo kwa amesema uongo bungeni na amewasingizia wanachi wa Karagwe mambo ambayo hawajafanya. Kama hataki kufuta kauli yake na kuwaomba msamaha wananchi hao, basi athibitishe ni kikao gani cha wananchi kilichokaa kuzungumzia katiba na kikaazimia kumtuma akubali muswada.
Great thinkers, suala la katiba si sawa na suala na barabara au maji au umeme ambalo mbunge anaweza tu kusema wananchi wangu wanataka.......!
Kwa kuwa najua Blandes hatafuta kauli yake kutokana na jeuri ya ccm, naomba mwongozo wa hatua za kisheria kumshtaki mbunge huyu, kumkataa ili uitishwe uchaguzi mwingine.