Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kamoli akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2024/25 leo Mei, 6, 2024 amesema ikiwa suala la fidia ya wananchi wa Kipunguni halitapatiwa maelezo ya kutosha, basi atashika shilingi na hataachia.
Amesema suala hilo limechukua muda mrefu wa takribani miaka 27 na hakuna jambo linaloendelea licha ya wananchi kupewa ahadi za kulipwa fidia zao mara kwa mara.
Mbunge huyo amesema hawawezi kwenda kuomba kura kwa mazingira waliyoyatengeneza wenyewe.
Pia, soma
Amesema suala hilo limechukua muda mrefu wa takribani miaka 27 na hakuna jambo linaloendelea licha ya wananchi kupewa ahadi za kulipwa fidia zao mara kwa mara.
Kamoli amesema mwaka jana alifatwa na waziri wa uchukuzi na kumwambia sasa wako tayari kulipa na wakaenda wote Kipunguni. Anasema Serikali ilisema itaanza kuwalipa mwezi wa tisa mwaka jana na kuwapa miezi mitatu kuhama baada ya siku ya malipo hivyo wananchi walianza kuvunja nyumba zao kuondoa wapangaji.Mbunge huyo amesema hawawezi kwenda kuomba kura kwa mazingira waliyoyatengeneza wenyewe.
Pia, soma
- Serikali: Tutaanza kuwalipa fidia wananchi wa Kipunguni waliopisha upanuzi wa uwanja wa ndege
- Wakazi wa kipunguni hawajalipwa fidia toka 2022
- Fidia ya Kipunguni A mbona danadana nyingi, TAA tuambieni ukweli
- Serikali imeanza kutekeleza hoja ya CAG ya kulipa fidia wakazi wa Kipunguni kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege JNIA
- Serikali walipeni wakazi wa Kipunguni kwa kuwa tathmini imekamilika
- Wakazi wa Kipunguni Dar es Salaam ambao tuliteseka zaidi ya miaka 20 mwaka huu tumefanyiwa tathimini ya majengo na ardhi. Tunasubiri malipo
- Bomoabomoa Kipunguni, Ukonga walipwe haki zao