Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Magharibi, Tauhida Cassian Galoss, amehoji udhibiti wa matumizi mabaya ya mitandao nchini, akieleza kuwa hali hiyo inaweza kuathiri amani na usalama wa taifa.
Akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Galoss alisema kuwa wakati vyombo vya ulinzi na usalama, ikiwemo Jeshi la Polisi, vinaendelea kutekeleza majukumu yao ipasavyo, changamoto kubwa sasa ipo kwenye mitandao ya kijamii.
"Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekuwa na uvumilivu wa kutosha, lakini imefika wakati. Mheshimiwa Waziri, kazi za ulinzi wa nchi hii zipo vizuri. Kazi ya Jeshi la Polisi kulinda mali na raia wake ipo vizuri. Tunashindwa sasa kudhibiti mitandao. Hatuwezi kuona nchi yetu inatawaliwa na mitandao. Jeshi la Polisi, angalieni kwa makini. Katika vitu vitakavyoweza kuleta dhoruba ni pamoja na mitandao. Mitandao sasa imekuwa ikitumika vibaya ndani ya Tanzania. Tunavumilia, lakini tumechoka."
Aidha, alilitaka Jeshi la Polisi kushirikiana kwa karibu na mamlaka nyingine ili kudhibiti maudhui hatarishi yanayosambazwa mitandaoni, akisisitiza kuwa taifa haliwezi kuruhusu mazingira ya mtandaoni kutumika kama kichocheo cha migogoro au uvunjifu wa amani.