Mbunge Cecil Mwambe ameidhihirishia dunia udhaifu mkubwa wa Tume ya Uchaguzi

Mbunge Cecil Mwambe ameidhihirishia dunia udhaifu mkubwa wa Tume ya Uchaguzi

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Tume ya Uchaguzi ( NEC) ndio husimamia na kuendesha chaguzi za Rais, wabunge na madiwani.

Vyama vya siasa ni wadhamini tu wa wagombea ambao kwa mujibu wa katiba ni lazima wawe wanachama wa vyama vya siasa.

Bunge kama muhimili ni chombo cha Wananchi ambacho hupokea majina ya wabunge ama wa kuchaguliwa au kuteuliwa kutoka Tume ya Uchaguzi. Baadae wabunge hao huapishwa na kuanza kuwatumikia wananchi.

Cecil Mwambe alipata ubunge kwa dhamana ya Chadema na kuapishwa kuwa mbunge akiwawakilisha wananchi wa Ndanda.

Baada ya miaka minne Cecil Mwambe akiwa na akili zake timamu kabisa aliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutangaza mosi kujiuzulu ubunge na nafasi nyingine za uongozi ndani ya chama, pili kujivua uanachama wa Chadema na tatu kujiunga na chama cha mapinduzi yaani CCM.

Sasa kiutaratibu lilikuwa ni swala la Mwambe kuijulisha NEC kwamba amejiuzulu ubunge, na NEC ndio wangemtaarifu Spika kwamba jimbo la Ndanda liko wazi baada ya mbunge wake kujiuzulu. Kadhalika Chadema wangefahamishwa kwamba dhamana yao kwa Cecil Mwambe imefikia kikomo baada ya mbunge huyo kujiuzulu ubunge kwa hiyari yake. Endapo Chadema wangekuwa na objection yoyote wangeiambia Tume ya Uchaguzi siyo ofisi ya Spika.

Kwa muktadha ni ama Cecil Mwambe amefanya siasa chafu zile ambazo Mwalimu Nyerere aliziita " Umalaya wa kisiasa " au Tume ya Uchaguzi iliteleza mahali fulani.

Katika hili huwezi kumlaumu Spika Ndugai kwa sababu yeye analetewa tu ama mpokee mbunge au jimbo liko wazi.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kuna wakati tukubali kwamba baadhi yetu tunatumia viungo vingine kufikiria hata kama viungo hivyo ni vichwa lkn tukubali tu sio vichwa vilivyo juu ya shingo
 
Siku zote NEC inataarifiwa na spika kuwa jimbo fulani lipo wazi na siyo kazi ya tume kujua jimbo gani lipo wazi. Na imani hata Nyalandu angekuwa ametoka Chadema akaenda CCM leo hii angeitwa, hii ni dharau kubwa sna kwa katiba ya nchi na wananchi wenyewe. Diwani imetolewa barua ya kufoji chama chake ngazi zote zinamtambua anasimama Waziri mvuta bangi anasema hamtambui diwani na bunge linashangilia, mbunge ambaye kautaa ubunge mchana kweupe na chama hakimtambui lakini anaitwa bungeni kwa mbwembwe kubwa. Shame on them
 
Viongozi walioapa kuilinda na kuitetea Katiba ya Nchi wanainajisi mchana kweupe.
 
Back
Top Bottom