Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge Cherehani Aiomba Serikali Kuwapa Wananchi Ruzuku ya Gesi
Mbunge wa Ushetu (CCM), Emmanuel Cherehani ameiomba Wizara ya Nishati kutoa ruzuku ya gesi kwa wananchi waishio maeneo ya vijijini, ili kusaidia utuzwaji wa mazingira na kuthibiti ukatwaji wa miti pamoja na kupunguza gharama za maisha kwa wananchi hao.
Cherehani amesema hayo, Alhamisi April 4, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2024/2025.
Cherehani amesema kutakuwa na mabadiliko ya utunzwaji wa mazingira iwapo wananchi watawezeshwa kutumia nishati ya gesi ambayo kwa sasa inapatikana kwa gharama kubwa.
“Niiombe wizara iweke ruzuku kwenye upande wa mitungi ya gesi, ili tuwasaidie wananchi wapunguze nguvu ya kukata kuni na tuongeze nguvu kwenye ruzuku,” amesema Cherehani.
"Suala la mikopo ya 10% kuna Halmashauri nyingi zilitekeleza vyema mpango huu zikaponzwa na Halmashauri chache ambazo hazikufanya vizuri, ningeomba ufanyike utafiti vizuri kabla ya kuendelea na zuio hili" - Mhe. Emmanuel Cherehani, Mbunge wa Jimbo la Ushetu
"Tunawapa wananchi wa vijijini mitungi ya gesi iliyojazwa, ikiisha wanatumia umbali mrefu sana pamoja na gharama kubwa kwenda kuijaza tena, serikali ilitazame hili" - Mhe. Emmanuel Cherehani, Mbunge wa Jimbo la Ushetu
"Niko tayari kuwapa nyundo TANROADS ili wazunguke kukagua ubora wa barabara zetu kama ambavyo walikuwa wakifanya zamani" - Mhe. Emmanuel Cherehani, Mbunge wa Jimbo la Ushetu