Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani ambekabidhi Baiskeli kwa Wakulima 40 wa Mfano kwa Zao la Pamba Halmashauri ya Ushetu, ambazo zitawawezesha kufuatilia mwenendo wa uzalishaji Pamba kwa Msimu huu wa kilimo 2024/2025.
Akizungumza wakati wa kukabidhi baiskeli hizo Cherehani amewahimiza Wakulima wa zao hilo kupanua Wigo wa Uzalishaji kwa wakati huu ambao Serikali inatengeneza Mazingira rafiki ya kuliongeza thamani.
Kwa upande wao baadhi ya Wakulima hao wameahidi Kwenda kuwa Mabalozi hai wa Pamba kwa kuwatembelea na kuwahamasisha Wananchi kuendesha Kilimo chenye tija kwao.
Baiskeli hizo zimetolewa na Serikali kupiti Wizara ya Kilimo ikiwa ni mwitikio wa Ombi la Mbunge Cherehani kwa Bodi a Pamba nchini ikiwa ni sehemu ya kutambua juhudi za Wakulima wa Zao la hilo walizozifanya katika Msimu uliopita wa Kilimo.