Mbunge Cherehani Asema Tumbaku Bora Huanzia Shambani

Mbunge Cherehani Asema Tumbaku Bora Huanzia Shambani

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

MBUNGE CHEREHANI ASEMA TUMBAKU BORA HUANZIA SHAMBANI​

Wakulima wa zao la Tumbaku hapa Nchini wameaswa kuzingatia kanuni bora za kilimo cha zao hilo ili kuzalisha kwa tija na kupata soko la uhakika kutokana na kuendelea kuimarika kwa bei katika masoko.

Rai hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Cherehani wakati wa zoezi la kukabidhi zawadi za pikipiki kwa wakulima waliofanya vizuri katika uwasilishaji wa tumbaku katika masoko ya Awali kwa kampuni ya alliance one.

Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani amekabidhi zawadi ya pikipiki 60 zilizotolewa na Kampuni ya Alliance one kwa Wakulima wa Tumbaku waliofanya vizuri katika uwasilishaji wa zao la tumbaku katika masoko ya awali.

Tukio hilo maalum limefanyika leo Mei 23, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa kampuni hiyo uliyopo katika wilaya ya Urambo Mkoani Tabora likijuisha Wakulima kutoka mikoa mbalimbali ya Kitumbaku.

Akizungumza mara baada ya kutoa zawadi hizo Mbunge Cherehani ameipongeza kampuni ya Alliance One kwa kutoa motisha kwa kwa wakulima hao na kuziasa kampuni nyingine kuiga mfano huo.

Kwa upande wake Msemaji wa kampuni ya alliance one wakili john magoti amesema kuwa zoezi la utoaji wa zawadi kwa wakulima ni endelevu lengo nim kutoa motisha kwa wakulima , huku wakulima wakiishukuru Serikali kwa kuboresha mazingira ya kilimo na kuahidi kuongeza uzalishaji zaidi.

Kampuni ya ununuzi wa Tumbaku ya 'Alliance One' imekabidhi pikipiki 60 zenye thamani ya shilingi milioni 168 kwa wakulima vinara wa uzalishaji wa tumbaku bora na kupeleka sokoni kwa wakati.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2025-05-25 at 14.52.15.mp4
    28 MB
Back
Top Bottom