Mbunge Cherehani awaasa madereva kupunguza bei ya nauli Kahama -Shinyanga

Mbunge Cherehani awaasa madereva kupunguza bei ya nauli Kahama -Shinyanga

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
"Niwaombe wenzangu wenye Hice (Daladala), Mabasi, Gari za Abiria kutoka Urowa kwenda Kahama zamani mlipandisha nauli kwasababu ya barabara mbovu. Kwanini msishishe nauli kuwasaidia wananchi!" - Mhe. Emmanuel Cherehani, Mbunge wa Jimbo la Ushetu Kahama-Shinyanga

"Kama kilio ilikuwa ni barabara, imetengenezwa. Kama ni mafuta, Mheshimiwa Rais ameshusha bei ya Mafuta. Maeneo mengine tunayosafiri bei zimeshuka. Kaeni chini mlifanyie kazi muwaangalie wananchi wanajichanga fedha kidogo, wanasafiri kwa shida, punguzeni bei" - Mhe. Emmanuel Cherehani, Mbunge wa Jimbo la Ushetu Kahama-Shinyanga

"Suala la Afya, kulikuwa na tatizo wagonjwa wanapoenda Hospitali hawapokelewi vizuri, lugha inakuwa ngumu, akina Mama wanaojifungua wanapojifungulia nyumbani wanaambiwa Shilingi elfu 50. Nashukuru tumeyashughulikia" - Mhe. Emmanuel Cherehani, Mbunge wa Jimbo la Ushetu Kahama-Shinyanga

"Kuna maeneo machache ambapo nimemuomba Mkurugenzi ayashughulikie hasa katika Kituo cha Afya Ukune bado kuna shida. Nimemuambia Diwani nitaenda Ukune kuonana na wauguzi wote, madaktari tuangalie mwenye tatizo ni nani tumuondoe kwenye Jimbo la Ushetu" - Mhe. Emmanuel Cherehani, Mbunge wa Jimbo la Ushetu Kahama-Shinyanga.


WhatsApp Image 2023-07-14 at 12.05.47(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-14 at 12.05.47(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-14 at 12.05.47.jpeg

 
Back
Top Bottom