Mbunge Cherehani: Ondoeni Tozo ya Mionzi kwa Wanunuzi wa Tumbaku

Mbunge Cherehani: Ondoeni Tozo ya Mionzi kwa Wanunuzi wa Tumbaku

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

MBUNGE CHEREHANI: ONDOENI TOZO YA MIONZI KWA WANUNUZI WA TUMBAKU​

Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Emmanuel Cherehani ameiomba Wizara ya Kilimo kuondoa tozo ya mionzi kwa nunuzi wa zao la Tumbaku, kwani inawaumiza sana wanunuzi ambayo inasababisha wakulima kupunguziwa bei ya kuuza zao hilo.

Pia ameshauri kuwe na mnada wa masoko ya tumbaku na mikataba ili kuweza kupiga hatua kama mataifa mengine yanavyofurahia, kwani wapo wakulima wenye uwezo wa kufanya kwa mnada na wasio na uwezo waingia katika mikataba.

Cherehani ameeleza hayo leo Mei 21 Bungeni Dodoma baada ya Wizara ya Kilimo kuwasilisha hotuba yake ya bunge la Bajeti mwaka 2025/26.

Awali, akizungumza hayo Cherehani amesema Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe alipokuwa Naibu Waziri alikuwa akitembea ofisi za wizara ya fedha kuondoa kodi na kufuta tozo kwa wakulima amabazo amefanikiwa kuziondoa kwa kiasi kikubwa.

Ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka minne ya Rais Samia Suluhu Hassan tozo 26 zimeondolewa katika zao la tumbaku, hivyo ameomba kuondolewa kwa tozo ya mionzo kwa wanunuzi kwani hasara inakuwa kwa wakulima kwa sababu wanunuzi wanapunguza bei kwa wakulima.

“Tukitoa tozo kwenye mionzi wanunuzi wanakwenda kumpelekea bei mkulima sasa tunatika kwenye dola 3 tunaenda kwenye dola 4 kwa L10F tunaenda kukimbizana na wenzetu Malawi na Zimabwe ambao wameenda kwenye dola 4 hadi dola 5,” amesema Cherehani.

Sambamba na hilo ameshauri zao la maembe liwekwe katika ushirika kwa kuanza kufanya tathmini ya maembe yanayovunwa kiholela vijijini ili yavunwe kwa utaratibu mzuri kwani itasaidia kuongeza na kuchangia mapato katika halmashauri.

Cherehani ameshauri benki ya Ushirika iliyozinduliwa Mwaka huu na Rais Samia isambazwe matawi nchi nzima ili kuwafikia wakulima wote nchini.

Katika hatua nyingine amempongeza Bashe kwa kutengeneza kura za Rais Samia kwa wakulima wote nchini kwa heshima kubwa kwa kiwango ambacho ni cha kimataifa ambacho ameitengeneza kwa wakulima wa mazao mablimbali.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2025-05-21 at 17.27.32.mp4
    36.7 MB
Back
Top Bottom