Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE CHRISTINA MNZAVA AGAWA VIFAA VYA MICHEZO KWA WANAFUNZI SHINYANGA VIJIJINI
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Dkt. Christina Christopher Mnzava amegawa vifaa vya michezo kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kaselya iliyopo katika Kijiji cha Igegu Kata ya Mwamala Wilaya ya Shinyanga Vijijini
Katika ziara yake, Mhe. Christina Christopher Mnzava amefanya mkutano wa hadhara katika Mtaa wa Majengo katika Kata ya Kambarage ndani ya Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kuelezea Utekelezaji wa Ilani ya CCM na kuwapa mrejesho wananchi kuhusu Bajeti Kuu ya Serikali ya Mwaka Mpya wa Fedha 2024/2025.
Aidha, Mhe. Christina Christopher Mnzava amefanya mkutano na Wanawake wa Kata ya Ntobo iliyopo katika Jimbo la Msalala kwa lengo la Kuhamasisha Wananchi wote Kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ili wapate haki ya kupiga kura wakati wa uchaguzi.
Mhe. Christina Mnzava amewaambia Wanawake watumie fursa na haki yao ya kuchagua na kuchaguliwa na wajitokeze kuwania nafasi kwenye Mitaa, Vitongoji na Vijiji ili kuwa uwakilishi wa Wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi.
Katika Mikutano yote ya hadhara aliyofanya, Mbunge Christina Mnzava ameendesha zoezi la
kusajiri wanachama wapya katika mfumo wa kielektroniki; Ameelezea mambo yaliyofanywa na Rais (Utekelezaji wa Ilani ya CCM); Kusikiliza kero na kuzifanyia kazi.