Mbunge Condester Michael atimuliwa Bungeni kwa kuvaa ovyo. Spika awaagiza askari wa bunge kuwazuia getini wavaa ovyo

Lakini hako ka suruali ka kichangu tu
 
Hoja zisizofanana.....

Suala la wao kutengeneza madawa tunayotumia na kanuni za mavazi za bunge la JMT Wala hazilingani.....

Hoja iliyo mezani je BUNGE HALINA KANUNI ZA MAVAZI ?!!!

Mbona maofisi ya serikali ,ikulu Kuna kanuni za mavazi...nako wanakosea kwa kuwa tu TUNATENGENEZEWA CHANJO NA MADAWA NA NCHI ZA NJE?!!!

Halafu unaumiaje na kanuni bunge walizojiwekea WENYEWE?!!!

BUNGENI ni sehemu ya kutunga sheria....si kila sheria ITUNGWAYO kwao wenyewe na kwa nchi ITARIDHIWA NA KILA MMOJA WETU.....

Mh.Spika JYN yu sahihi....

#KaziIendelee
 
Wewe ndio utakua na matatizo ya akili
Huyo mbungwe wenu ni dinasour!
Ni wazi hastahili kuwa bungeni, kwani mizigo ya mawaziri wa kike haioni bungeni?
Mshaurini kuwa bungeni si genge la kijiwe cha kahawa kujadili wanawake walivyotokelezea na mixigo yao!
Apevuke kiakili.
 
Halafu badae Mbunge mwengine Mama mtu mzima anasimama na kutetea uvunjwaji wa maadili ya kitanzania na kanuni za Bunge nila hata aibu!!!
huyu Bibi nae anapaswa apumzishwe nyumbani.
Spika asipo simama Imara Bunge hili litapoteza heshima yake kabisa
 
Huyo mbungwe wenu ni dinasour!
Ni wazi hastahili kuwa bungeni, kwani mizigo ya mawaziri wa kike haioni bungeni?
Mshaurini kuwa bungeni si genge la kijiwe cha kahawa kujadili wanawake walivyotokelezea na mixigo yao!
Apevuke kiakili.
Bungeni kunajadiliwa VINGI TU...mpaka Simba na Yanga....

Hoja....je mjadala wake wa JANA ulikuwa ni wa "kijiwe cha kahawa" usio na rejea ya KANUNI NA SHERIA ZA BUNGE?!!

Je mjadala wake wa "kijiwe cha kahawa" ndio ulikuwa ni SHERIA NA KANUNI zilizomtoa nje Yule MBUNGE mwanamke?!!!

Je huyu mh.Amar ndiye aliyemtoa nje huyo mbunge mwanamke?!!!!

#KaziIendelee
 
Yafuatayo ni maeneo ya Heshima na hivyo yanataratibu zake;
1. IKULU

2. BUNGENI

3. JESHINI

4. MAHAKAMNI.

Hayo maeneo na matukufu na yana taratibu zake, huwezi kupita au kuingia ktk maeneo hayo na mavazi yasiyo na heshima lazima utaondplewa au utazuiwa.

kinacho tokea hivi sasa ni ukosefu wa maadili kwa baadhi ya wabunge wetu.
 
Hivi huyu dada ametolewa nje na mbunge aliyeomba mwongozo kwa spika,au ametolewa nje na mwongozo wa spika?
Na kama kuna sheria ya mavazi bungeni,huyu dada aliisoma au hawajapewa miongozo kuhusu mavazi?
 
Hili sio vazi rasmi la mtumishi wa umma akiwa ofisini!

Sent from my TECNO-W3 using JamiiForums mobile app
Tofautisha Mtumishi wa Umma na Kiongozi wa Umma (Public Servant Vs. Public Leader ).

Sheria zinazowa-govern ni tofauti, code of ethics and conduct tofauti, maagizo na makatazo tofauti.

Kadhalika kanuni za mavazi tofauti, bunge wana zao na utumishi walitoa zao kwa Waraka.

So punguza mihemko. Pole Dada Mbunge umeonewa.
 
Hakuna Bunge ninalolidharau kama la sasa.
Mabunge yote yamepita kwa Wizi na Ulaghai wa Mwendazake
 
Tatizo Ni kutovaa ushungi
 

Mkuu Acha kufananisha mambo ya tamaduni. La msingi Tuone Nini kinafaa kwa watanzania.
 
Ha ha ha!!!! Anakwazwa na masanamu!!!! Ana shida huyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…