Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE CONDESTER SICHALWE AISHAURI WIZARA YA KILIMO KUFUNGUA DIRISHA ILI KUPATA PEMBEJEO ZA KILIMO MAPEMA
Mbunge wa Jimbo la Momba Mkoa wa Songwe Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni ameuliza swali Wizara ya Kilimo ambalo lilijibiwa na Naibu Waziri Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde
"Je, Wizara ya Kilimo inaonaje kwamba ikitumia muda huu kufungua dirisha la kuwakopesha wakulima Mbegu, Mbolea, Viuatilifu na vitendea kazi vingine ili kujiandaa na msimu wa Kilimo unaokuja?" - Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe
"Hivi sasa Wizara ya Kilimo kupitia Wakala wa Mbegu tupo katika utaratibu wa kuanza kusambaza Mbegu kwa msimu unaokuja kwa kufungua Madirisha kupitia maeneo tofauti tofauti. Vilevile tunao mfuko wetu wa Pembejeo ambao ni mahususi kwa ajili ya kuwasaidia wakulima kuweza kupata Pembejeo kwa wakati na kwa bei nafuu." - Anthony Mavunde, Naibu Waziri Kilimo
"Nichukue fursa hii kuwaomba wakulima wote nchini Tanzania kutumia Madirisha yote Mawili kwa ajili ya kuweza kupata Pembejeo hizo kwa wakati ili wakati wa msimu wawe tayari wanazo na kuanza kutumia kwa ajili ya Kilimo" - Anthony Mavunde, Naibu Waziri Kilimo