Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Momba Condesster Sichalwe ameishauri Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Wizara ya Uchukuzi waone namna ya kushirikiana na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) ili kujenga barabara ya kulipia ambayo itaongeza Pato kwa Taifa.
Sichalwe ametoa ushauri huo bungeni jijini Dodoma, wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025.
"Mimi situmii pombe ila niliongea na mtumia pombe mmoja nikamuuliza kuhusu pombe ya Amarula akaniambia inatengenezwa kwa kutumia maziwa yaani ng'ombe wote wa Mhe Ulega walioko hapa nchini ambao tunaweza tukakamua maziwa ya kutosha kweli tumeshindwa kuchukua gongo ya Watanzania tukachukua na maziwa yetu tukatengeneza na sisi tukapata Tanzaniarua yetu ili watu wakajua hii imetoka huko na hii ni pombe yetu kutoka kwenye maziwa yetu wenyewe lakini kutoka kwenye gongo yetu wenyewe," - Condester Sichalwe
"Mhe Waziri (Viwanda na Biashara) hii ni karibu mwaka wa nne nakupa hoja hiyo hiyo yaani nyie hamna mtambo kweli wa kutenganisha Methanol na Ethanol kwenye gongo ili kiwe kinywaji halali kitumike, nimeshaongea na watu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakasema wana maandiko mengi kuhusu gongo si muende mkakae nao wawasaidie ili gongo iweze kuhalalishwa?," - Condester Sichalwe