Mbunge Condester Sichalwe - Uzeni Mazao wa Utaratibu, Njaa Bado Ipo Tanzania

Mbunge Condester Sichalwe - Uzeni Mazao wa Utaratibu, Njaa Bado Ipo Tanzania

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MBUNGE CONDENSTER SICHALWE AWAASA WANANCHI KUUZA MAZAO YA CHAKULA KWA UTARATIBU, NJAA BADO IPO

Mbunge wa Jimbo la Momba Mkoa wa Songwe Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe leo tarehe 22 Julai, 2023 amezungumza na wananchi wa Kijiji cha Iyendwe Kata ya Kapele na kuwasisitiza kuuza mazao ya Chakula kwa utaratibu mzuri kwani njaa bado ipo.

Mhe. Condester Sichalwe ameyasema hayo katika Kijiji cha Iyendwe baada ya kuhudhuria msiba wa aliyekuwa baba yake mkubwa Ndugu Sichalwe (76) uliotokea tarehe 21 Julai, 2023 baada ya kupata matibabu Hospitali ya Vwawa na kushindikana.

Mhe. Condester Sichalwe amewasisitiza wananchi wa Iyendwe kujitokeza kwa wingi kujiandikisha majina ya kupata mbole ya ruzuku inayotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia mabwana shamba wanaopita kuchukua idadi ya wakulima ili wapate mbolea ya ruzuku bure.

Mhe. Condester Sichalwe amesema kuwa Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imetenga fedha kwaajili ya ujenzi wa Skimu ya umwagiliaji hivyo amewaomba wananchi kuhudhuria vikao vya kupewa Elimu ya umwagiliaji inayotolewa na tume ya umwagiliaji kwenye Vijiji na Vitongoji vyao.

Aidha, Mhe. Condester Sichalwe amekemea vikali vitendo vya kuchoma moto mashamba yenye mazao kwani kumekuwa na kesi nyingi kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji juu ya kuchomeana mashamba kwani muda wa mavuno bado haujaisha hivyo wananchi wawe makini wanapowasha moto wa kupikia mashambani.

Mwisho, Mbunge Condester Sichalwe amewashukuru wana Kijiji cha Iyendwe kwa faraja katika msiba wa baba yake mkubwa na kuwakumbusha kupima afya mara kwa mara ili magonjwa yanayoepukika yapatiwe tiba na kuepusha vifo visivyo vya lazima katika Kijiji cha Iyendwe.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-07-23 at 00.06.21.mp4
    15.2 MB
  • WhatsApp Video 2023-07-23 at 00.05.48.mp4
    8.5 MB
Back
Top Bottom