Mbunge David Kihenzile Achangia Milioni 10 Ujenzi Ofisi ya Kata Igowole

Mbunge David Kihenzile Achangia Milioni 10 Ujenzi Ofisi ya Kata Igowole

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MBUNGE DAVID KIHENZILE ACHANGIA MILIONI KUMI UJENZI WA OFISI YA KATA YA IGOWOLE- MUFINDI KUSINI

Mbunge wa Mufindi Kusini David Kihenzile amefanya Kikao cha pamoja kilichojumuisha Viongozj wote wa Kata ya Igowole ikiwemo Wajumbe Mkutano Mkuu CCM Kata, Mabalozi, Vitongoji, Viongozi wa dini, Wafugaji, Wavuvi, Wazee w Mila, Watumishi wa Serikali pamoja na makundi mengine Muhimu.

Katika Kikao hicho pamoja na mambo mengine alifafanua kazi zikizofanyika na zinazoendelea kufanyika kwenye Kata hiyo ikiwa ni pamoja na Mradi wa Maji, ujenzi wa Shule Mpya 6, Upanuzi na utoaji Vifaa vya hospitali ya Wilaya pamoja, Ujenzi barabara ya lami za Nyololo na Ile ya Mgololo.

Aidha Mbunge akechangia Bati 120 zenye thamani ya takribani milion 5 na Pesa Milion 5 ili Kuunga Mkono Ujenzi huo uliopanga kugharimu Tsh milioni 29.

Kihenzile anaendelea na ziara Jimbon kwake ambapo pamoja na kuzungumza na viongozi mbalimbali, Mikutano ya hadhara lakinj pia ameanzisha Program ya Kujenga Chama kwa Kuendelea kuhamasisha ujenzi wa Maofisi na kuanzisha Mkakati wa Ugawaji Kadi za CCM 50,000 kwa mabalozi wa Shina.
WhatsApp Image 2023-07-23 at 00.33.52(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-23 at 00.33.52.jpeg
WhatsApp Image 2023-07-23 at 00.33.53(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-23 at 00.33.55.jpeg
 
Back
Top Bottom