Ndo katoa vile virikuu?Mbunge wa Same Magharibi Mh David Mathayo amekabidhi magari ya wagonjwa kwa kila kata katika jimbo lake.
Mathayo amesema magaru hayo imara sana ameyanunua yeye mwenyewe ili kuwasaidia wapiga kura wake na hasa akina mama ukizingatia Same ni eneo lenye milima.
Source: Upendo TV
Maendeleo hayana vyama!
Daah! Waswahili bana mwingine alitoa magari ya kubebea maiti watu wakaanzaa oooh anaacha kutoa gari ya wagonjwa anatoa ya maiti haya huyu nae anajitolea gari la wagojwa mmekuja na jingine.Anaacha kujenga viwanda watu wapate ajira ili wajitibu wenyewe, anatoa magari ya wagonjwa kana kwamba wakazi wote wa huko kwake ni wagonjwa!
Anaacha kujenga viwanda watu wapate ajira ili wajitibu wenyewe, anatoa magari ya wagonjwa kana kwamba wakazi wote wa huko kwake ni wagonjwa!
Kwahili mkuu (umeghafirika)......bila shaka utakuwa umezaliwa na kukulia hapo ilala boma.......kama yataenda kutumika vizuri yatasaidia wengi sana katika hayo maeneo......kuna vitu tupongeze mtu anapofanya jambo kwa maslahi ya jamiiAnaacha kujenga viwanda watu wapate ajira ili wajitibu wenyewe, anatoa magari ya wagonjwa kana kwamba wakazi wote wa huko kwake ni wagonjwa!
Mbona 2015 hadi 2020 wakikuwa wanakamatwa wakitoa hiyo misaada??Kumbe binadamu ni kazi kuwaridhisha,kuwapa watu magari ili ikitokea mtu kazidiwa awahishwe kwenye matibabu kumbe ni zambi?
Kwahili mkuu (umeghafirika)......bila shaka utakuwa umezaliwa na kukulia hapo ilala boma.......kama yataenda kutumika vizuri yatasaidia wengi sana katika hayo maeneo......kuna vitu tupongeze mtu anapofanya jambo kwa maslahi ya jamii
Zitumie basi kufikiria ili uone kwamba hata sisi huku vijijini tunastahili kupata huduma ya kuwahishwa hospitali tukizidiwa badala ya kwenda kwa bodaboda. Tatizo lenu watu wa mjini huwa hamtufikirii sisi walala puu wa huku vijijini: sisi tunapata magari ya kutuhudumia, wewe unaona hiyo hduma haitustahili!Ameshanirudishia, ila majizi ya kura huwa sijipendekezi nayo.
Mkuu kata zaidi ya kumi ndio ngapi?Kata zaidi ya kumi!