The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mbunge wa Jimbo la Tunduma, David Silinde, amewapa ujumbe mzito wanaotamani kugombea nafasi yake katika Uchaguzi Mkuu ujao, akisisitiza kuwa maendeleo makubwa yaliyofanyika chini ya uongozi wake yanampa uhakika wa ushindi mkubwa yeye na Rais Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza jana Februari 22, 2025, mbele ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Fadhili Mganya, katika ukumbi wa High Class Tunduma, Silinde alisema yeyote anayejiona kichwa ngumu anakaribishwa kuwania, lakini atakutana na uhalisia wa siasa za Tunduma.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Hakuna cha kubahatisha hapa! Kila kata tumetekeleza miradi mikubwa, tumeshajenga shule 27,tuna shule za ghorofa za kutosha tena bila kuchangisha mwananchi hata shilingi moja. Hivi kweli mtu anaweza kupita hapa bila kuona maendeleo? Tunduma tunatembea kifua mbele!" alisema huku akishangiliwa.
Silinde aliwataka wanaojipanga kugombea kujiandaa vizuri kwani wapiga kura wa Tunduma hawadanganyiki na kwamba CCM chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaungwa mkono kwa nguvu kubwa.
Kauli yake ilizua shangwe ukumbini kwa zaidi ya dakika mbili, ishara kuwa wanachama wa CCM wana imani kubwa na kazi yake jimboni humo.